Social Icons

Wednesday, May 11, 2011

MISS MWANZA KUZINDULIWA

UZINDUZI wa shindano la urembo kumsaka Miss Mwanza 2011, ulifanyika
Juni Mosi, mwaka huu kwenye ukumbi wa Hoteli ya Kitalii ya Gold Crest iliyopo
katika jengo la PPF, katikati ya Jiji la Mwanza.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Sisi Entertainment, waandaaji wa shindano
hilo, John Dotto, alisema uzinduzi huo umeambatana na utambulisho wa warembo
watakaochuana katika kinyang’anyiro hicho.
Alisema kuwa tayari warembo wameshaanza kujiandikisha kuwania Umalkia wa Mwanza
na kwamba wanaojiona kuwa na sifa za kushiriki mashindano hayo, wanakaribishwa
ambapo fomu zinapatikana katika ofisi za hoteli hiyo.
“Bado tunakaribisha warembo wenye sifa kujiandikisha kwa sasa kwani baada ya
uzinduzi, hatutapokea mrembo yeyote yule, hata awe na sifa kiasi gani,” alisema.
Alisema kuwa shindano lao linatarajiwa kuwa la kiwango cha juu, kuanzia
maandalizi yake, warembo na shoo ya kilele cha kinyang’anyiro hicho.

0 comments: