Daladala lililopata ajali likiwa eneo la tukio.
WATU wawili wamefariki na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa leo asubuhi jijini Dar es Salaam baada ya basi dogo aina ya Toyota DCM linalofanya shughuli za kusafirisha abiria (daladala) kati ya Kigogo Mburahati na Kivukoni jijini Dar es Salaam, kupinduka eneo la Kigogo Festini.
Baadhi ya wananchi waliofika kushudia ajali hiyo.
Kutokana na kutofunguka kwa mlango wa dharura, Wasamaria walivunja kioo cha mbele ili kuwachomoa majeruhi.
0 comments:
Post a Comment