Social Icons

Wednesday, April 6, 2011

VIONGOZI WA SERIKALI WATEMBELEA MAONESHO YA HARUSI

Mustafa Hassanali akibadilishana mawazo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Mh.William Lukuvi (kulia).
Naibu waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mh. Ummy Ally Mwalim akisaini kitabu cha wageni jana kwenye moja ya mabanda ya maonyesho ya Harusi yanayoendelea katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Mambo ya Malaika Event Rentals.



MAONYESHO ya Harusi 2011, yaliyodumu kwa takriban siku tatu mfululizo toka tarehe 1 mpaka 3 mwezi April yamemalizika rasmi jana katika ukumbi wa Diamond Jubilee, huku yakiwa yamefikia malengo kwa asilimia kubwa zaidi ya yale ya mwaka jana.

Akizungumza katika kuhitimisha maonyesho hayo, muaandaaji na muasisi wa maonyesho hayo Mustafa Hassanali alisema kuwa, wamefanikiwa kwa asilimia kubwa kwa yale yote walioyapanga, na kufanya maonyesho ya mwaka huu kuwa na vionjo kadha wa kadha.

“tulipanga mengi kuyafanya katika maonyesho ya Harusi kwa mwaka huu, na mengi hayo yamefanikiwa kwa mwaka huu, hii imetupa faraja ya kuanza kujipanga kwa mwaka ujao. Ni kazi ngumu kuandaa maonyesho makubwa kama haya, ila kwa kuwa tulihitaji kuwaweka pamoja wafanyabiashara na wajasiriamali wa kazi za Harusi, ilibidi tufunge mkanda kukamilisha.”alisema Mustafa Hassanali.

Maonyesho hayo ya Harusi yaliweza kuwakusanya zaidi ya wafanyabiashra 51 walioonyesha bidhaa zao, kupata mtandao wa kibiashara kwa kukutana na afanyabiasharawengine, pia wateja waliokuja kununua na kujionea mambo mbalimbali katika ukumbi huo, bidhaa zilizoonyeshwa katika maonyesho hayo ilikuwa ni pamoja na magauni ya Harusi, mapambo, keki, picha na bidhaa nyingi zizokamilisha Harusi kwa ujumla.

Baraka ya maonesho hayo ilipatikana ambapo baadhi ya waliotembelea maeneo hayo ili kujionea ubunifu na umakini wa kibiashara za Harusi, ilikuwa na watu muhimu toka serikalini na sekta binafsi, ambapo wa kwanza kufika katika maonyesho hao alikuwa Mh. John Lukuvi, waziri katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo alifuatiwa na Mh. Ummy Ally Abdalla, naibu waziri wa Maendeleo Jinsia na Watoto ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kukamilishwa na Meya wa wilaya ya Ilala, Mh. Jerri Slaa ambapo yeye alitembelea maonyesho hayo siku ya tatu na ya mwisho ya maonyesho hayo.

Kwa nyakati tofauti ndani ya maonyesho hayo, waheshimiwa hao walisifu jitihada zinazofanywa na mbunifu huyo wa mavazi Mustafa Hassanali na kusema kuwa ni mjasiriamali wa kuigwa kwa mifano mizuri anayoitoa kwa jamii.

“kwa kweli Mustafa amefanya kitu cha kipekee, anastahili sifa kwa kuwa mfano wa kuigwa, hii inawapa wafanyabiashara na wale wa mapambo kama keki nafasi ya kujifunza na kujitangaza “ alisema Naibu Waziri wa Maendeleo, jinsia na watoto, Mh. Ummy Ally Mwalim.

Maonyesho ya mwaka huu yalijawa na ubunifu wa hali ya juu, huku mambo kemkem mapya yakijitokeza katika maonesho hayo.
Mbali na kuzinduliwa kwa jarida la kwanza na la kipekee la masuala ya Harusi, linalokwenda kwa jina la ‘Tanzania HARUSI Magazine’ lililochini ya Mustafa Hassanali, pia maonesho ya mwaka huu yaliongezewa nakshi ya midahalo kadha wa kadha ya mambo ya Harusi, moja ya watu mashuhuri waliotoa mada katika midahalo hiyo ni pamoja na Taji Liundi ambae alizungumzia kwa kina suala .kona ya wanaume, ambapo aligusia vitu mbalimbali yakiwemo masuala ya Harusi na mwanaume, hii ni pamoja na maandalizi na kabla na baada ya Harusi.

Ingawa yalikuwa mengi ya kuvutia, ilahayo yalikwa ni makubwa katika mwka huu wa maonesho ya Harusi.

Mustafa Hassanali aliweza kuwashukuru wadhamini na vyombo vya habari katika kuupasha umma habari zilizojiri katika siku zote tatu ambazo maonesho yaliendelea.

“kwa kweli tunaamini katika mchango mkubwa ambao vyombo vya habari umetupatia, waliokuwa mstari wa mberle katika kuhakikisha umma unahabarika katika kila taarifa ya maonesho haya, na kila aliyesikia naamini alijitokeza kutembelea maonesho haya” alimalizia Hassanali.
Maonyesho haya ya harusihufanyika kila mwaka, ambapo huu ni mwaka wa pili toka yameanza rasmi mwaka jana chinbi ya kampuni ya 361 Degrees ya Mustafa Hassanali.




0 comments: