Social Icons

Friday, April 8, 2011

MKURUGENZI WA GLOBAL AWAPONGEZA WAFANYAKAZI


Eric Shigongo (kulia) akimtia moyo mmoja wa wafanyakazi wapya wa kamopuni hiyo, Gladness Mallya.

MKURUGENZI wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo, leo amezungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo na kuwapongeza kwa utendaji waowa kazi, na kuwakaribisha na kuwatambulisha rasmi wafanyakazi wapya. Katika mkutano huo, kiongozi huyo aliahidi kuwaongezea maslahi wafanyakazi wake na kuboresha mbinu za utendaji wa kazi katika k ampuni hilo ambalo huchapisha magazeti ya Uwazi, Championi, Risasi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda na Amani.
Msanifu kurasa wa kampuni hiyo, Ally Kaskasi (kushoto), akitoa maoni yake na kuwashukuru wanafanyakazi wenzake kwa ushirikiano waliompa na kumuongezea uwezo wa kazi.

Mtaalamu wa Kitengo cha Kompyuta wa Global Publishers, Clarence Mulisa (kulia), na Mhariri, Walusanga Ndaki, wakisikiliza.

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdalah Mrisho, akisisitiza masuala yaliyozungumzwa na Mkurugenzi.

Mkurugenzi wa Global akiwa kwenye pozi na mwandishi wa Global Publishers, Shakoor Jongo ajulikanaye pia kwa jina la utani la ‘Zungu Fedha’.

0 comments: