Ndugu Zangu,
TAARIFA zimetufikia, kuwa Mwenyekitiki wa CCM, Jakaya Kikwete amevunja
CC na Sekretariati nzima ya CCM.
Tafsiri yangu; haya ni mabadiliko makubwa ndani ya CCM tangu kuundwa
kwake mwaka 1977. Mabadiliko makubwa ya kichama yalifanyika mwaka huo
wa 1977, wiki mbili tu baada ya CCM kuundwa.
Kuvunjwa kwa CC na Sekretariati kuna tafsiri kadhaa za haraka. Angalia
hapa, ina maana; CCM imeondokana na Rostam na Chenge kwenye CC. Wawili
hao hawarudi tena kwenye CC mpya itakayoundwa. Ndio, CCM wana namna
zao za ’ kufukuzana’ wanapoacha ' kulindana'.
Na hiki ndio kile tulichoambiwa; Chama Kujivua Gamba, au labda
magamba. Na kuna changamoto kwa Mwenyekiti wa Chama hicho- Unafanyaje
na magamba yaliyovuliwa? Unayafukia, au unayaacha yakitapakaa? Na
Magamba mengine hayaozi!
Ndio, Uchaguzi uliopita ulikuwa na ujumbe mmoja mkubwa kwa CCM kutoka
kwa wapiga kura. Ni huu; MABADILIKO. Ndio, Watanzania wanataka
mabadiliko. Kilichotokea Dodoma jana usiku ni jaribio la CCM kujibu
matakwa ya wananchi. Je, wamefaulu? Tuna sababu ya kusubiri huku
tukipima upepo unavyovuma.
Kuna maswali pia ambayo hatujapata majibu yake. Moja ni hili; Je,
Mabadiliko haya ndani ya CCM yana ukubwa na athari gani kwa wakati huu
na ujao?
Yepi zaidi yanakuja?
Tegemea- Kuwa asubuhi hii JK atakuwa ’ busy’ akishauriana na ’ wazee’
akina Msekwa, Mwinyi, Malecela, Mkapa na hata Spika Makinda. Wamsaidie
mawazo katika kupendekeza majina kama 26 hivi yatakayopelekwa kwenye
NEC ili yapigiwe kura na kupatikana wajumbe 18 wa CC.
Tegemea- Kuwa mengi ya majina hayo yakayopendekezwa yatatokana na
wajumbe vijana wa NEC.
Nani atakuwa Katibu Mkuu?
Tegemea- Kuwa Katibu Mkuu atakuwa ama kijana au ana sura ya kijana.
Jina kama Emmanuel Nchimbi si la kulibeza, William Lukuvi si ana sura
ya kijana?
Kwa yanayotokea Dodoma CCM itakuwa imemaliza kazi ya ’ kujibua’ au
kujivua gamba?
HAPANA. Kazi hiyo lazima iendelee. Kwa vile Sekretariati itaundwa
upya, basi, kutakuwa na sura nyingi mpya. Tegemea, kuona vijana wengi
zaidi wakipewa nafasi kwenye Sekretariati. Makatibu Wakuu wengi wa
Mikoa na Wilaya watapanguliwa. Na vijana wenye fikra za ’ kizamani’
nao watapotea, na hapa, Tambwe Hizza laweza kuwa ni jina la ’
vijiweni’ kule Temeke Mikoroshini. Na kuna wengi ndani ya CCM
wanaofanana na Tambwe Hizza.
Na upi ni mtihani mgumu kwa JK kwa sasa?
KATIBA MPYA, KATIBA MPYA, KATIBA MPYA….. ! Ndio, Watanzania wengi wa
sasa na hususan vijana wanataka MABADILIKO, na Katiba kwao ni sehemu
muhimu ya mabadiliko hayo. Watanzania wameshaamka na kubaini, kuwa
KATIBA yao ya sasa nayo ni ’ Maghumashi’. Neno hilo la mitaani lina
maana ya mambo ya kiini macho na ubabaishaji.
Kwa vile JK ameshawajengea matumani ya kuwasaidia kupata Katiba Mpya
itakayokidhi matakwa ya wakati uliopo na ujao, basi, nao wanataka iwe
hivyo. Na kama JK atataka abaki akikumbukwa hata na vizazi vijavyo,
basi, awe na ujasiri wa kuwasaidia Watanzania kupata KATIBA MPYA
itakayolifanya taifa hili liwe la kisasa na lifanye mambo yake ikiwamo
chaguzi katika mazingira ya kistaraabu. JK ana lazima ya kuacha
kuiangalia kwanza CCM na bendera yake, badala yake aingalie kwanza
Tanzania na bendera yake. Maslahi ya Nchi Kwanza. Maana, tunakokwenda,
hata ndugu wa JK wanaweza wasiipigie kura CCM.
Na walioandaa Muswaada wa Sheria ya Kuanzisha Mchakato wa Katiba
kimsingi wamechangia kumpunguzia JK heshima yake. Muswaada ule ni wa
kiwango cha chini sana. Na JK akikubali kuasisi mchakato wa Katiba kwa
kufuata ’ ramani’ ile tulioletewa juzi na kuambiwa tuitolee maoni,
basi, nahofia, kuwa kuna watakaosema mitaani; ” Na JK naye ni
Maghumashi!|”
Maggid
Iringa,
Jumapili, Aprili 10, 2011
0788 111 765

0 comments:
Post a Comment