
Habari za chini ya kapeti zinadai kuwa, staa wa filamu za Kibongo, Steven Charles Kanumba na Miss Ilala, 2009, Sylvia Shally ambao wanadaiwa kupeana ‘kampani’, wapo katika mtifuano mzito na sasa ishu yao imetinga Kituo cha Polisi, Oysterbay Kinondoni, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, ishu hiyo iliyosababisha pakachimbika ilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar.
Inasemekana kwamba, Sylvia ndiye anayedaiwa kumfikisha Kanumba kituoni hapo akilalamika kwamba, alimtishia maisha kupitia ujumbe mfupi wa simu ya mkononi (sms).
Kwa mujibu wa chanzo hicho, kabla ya tukio hilo, wawili hao walitibuana kufuatia kutoelewana kwa suala la kimapenzi ambalo halijawekwa wazi.
Kanumba hajamtumia demu wake meseji hiyo, walianza kupishana lugha kwenye uhusiano wao, ndiyo jamaa akaja juu,” kilisema chanzo.
Kikaendelea kudai kuwa, baada ya Sylvia kulifikisha suala hilo polisi, Kanumba aliitwa na ‘kusomewa’ shitaka lake lakini hakuonesha kukiri wala kukataa.
Inadaiwa kuwa, afande anayepeleleza kesi hiyo (jina tunalo) aliwataka wawili hao wakakae chini na kuondoa tofauti zao kisha warudishe majibu Jumatatu ya Aprili 18, mwaka huu.
Hata hivyo, chanzo kinasema, mpaka siku inakatika Jumatatu, wawili hao hawakurudi kituoni hapo kuelezea walikofikia baada ya ushauri wa afande.
Baada ya madai hayo, Jumanne ya Aprili 19, mwaka huu, mwandishi wetu aliamua kuwasaka wapenzi hao kwa njia ya simu zao za mikononi ili kuupata ukweli.
Saa nne asubuhi, Kanumba ndiye aliyekuwa wa kwanza kupigiwa simu ambapo iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
Alipogeukiwa Sylvia, naye simu yake ya kiganjani iliita kwa kitambo bila majibu.
Hata hivyo, paparazi wetu aliendelea kufanya jitihada za kuwapigia simu mara kwa mara lakini hakuna aliyepokea.
Ilipofika saa nane mchana, kila mmoja kwa wakati wake, walipigiwa tena simu na hakuna aliyeipeleka sikioni kutaka kujua kulikoni.
Saa tisa alasiri, mwandishi wetu aliamua kumtumia ujumbe mfupi (sms) Kanumba akimtaka apokee simu huku akijtambulisha kwa majina yote na anakofanyia kazi.
Baada ya hapo, simu hiyo ilipigwa tena, ikapokelewa na mtu aliyejitambulisha kwa jina la Kiuno ambaye alidai mwenye simu (Kanumba) alikuwa ‘shuting’.

Kama vile haitoshi, mwandishi kabla ya kupiga tena, alimtumia Kanumba ujumbe mfupi akimwelezea ‘shitaka’ lililo mezani kwake.
Baada ya meseji hiyo kuonesha imefika, mwandishi alitwanga simu, ikapokelewa na Kiuno yule yule ambapo alisema:
“Jamaa sijamwambia bwana. Lakini pia nimeona meseji, nikampelekea simu, alipoisoma akasema ‘si kweli.’
Baada ya kugonga mwamba kwa Kanumba, mwandishi alimtumia meseji Sylvia, akajaribu kumwelezea kisa kamili kutoka kwa chanzo chetu makini, lakini mrembo huyo hakujibu meseji wala kupiga simu achilia mbali ‘kubipu’.
Hivi karibuni, mmoja wa marafiki wa Sylvia alikaririwa akisema kuwa, mapenzi kati ya wawili hao yameingia nyongo.
Rafiki huyo (jina tunalo) alisema kuwa, Kanumba ni kama amemtosa Sylvia kwani hana ukaribu naye tena kama zamani, jambo ambalo linamkosesha raha mrembo huyo.
“Yaani naweza kusema kuwa, Sylvia anajua penzi la Kanumba kwake halipo, anasema ule ukaribu kama zamani hakuna tena, anakosa raha kabisa,” alisema rafiki huyo.
0 comments:
Post a Comment