Social Icons

Thursday, April 21, 2011

HAMMIE RAJAB AZIKWA, AACHA SIMANZI!


Hatimaye Mzee Hammie Rajab amezikwa mkoani Morogoro jioni hii, katika maziko yaliyofanyika katika makaburi ya Kola, mkoani humo. Hammie amecha simanzi kubwa kwa wasanii, ambao wengi wao wamekosa nafasi ya kumuaga na kumzika baada ya kuchelewa kupata taarifa zake za kifo na kushindwa kusafiri kwenda Morogoro kwa maziko. Idadi ya watu waliohudhuria makaburini ilikuwa ndogo kwa sababu mara baada ya mwili kuwasili mjini Moro, wanafamilia walielekea makaburini baada ya muda mfupi. Mungu ailaze roho ya marehemu peponi - Amin.

waombolezaji wakielekea makaburini

...shughuli ya maziko ikiendelea

..hapa ndiyo mwanzo wa makazi yake mapya ya milele

...baada ya maziko, nasaha za sheikh zilifuatia


...Rais wa Wasanii wa Shirikisho la Filamu nchini, Bw. Mwakifamba aliwakilisha wasanii wenzake katika maziko hayo.

0 comments: