Social Icons

Monday, April 25, 2011

BONGO INATISHA



Huku Pasaka ikiwa inaishia-ishia zake, matukio kibao ya kutisha yalijiri ndani ya Jiji la Dar huku wengi wakisingizia ni sherehe za sikukuu hiyo.

Katika tukio la kusikitisha, mtu mmoja mwanaume aligongwa na gari na kufa kwa kufumuliwa ubongo alipokuwa akivuka barabara maeneo ya Victoria.

Tukio hilo lilijiri Ijumaa, Aprili 22, mwaka huu ambapo Wakristo duniani kote walikuwa wakikumbuka mateso ya Bwana Yesu Kristo.

Mkononi mtu huyo alikuwa amebeba chipsi kwenye mfuko wa rambo ambazo zilizagaa eneo la tukio mara baada ya ajali hiyo.

MUME AKESHA MLANGO WA GESTI KUMSUBIRI MKEWE
Huko Buguruni, nje ya gesti moja ambayo tunaihifadhi jina, mwanaume mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Baba Sarah, alitumia usiku kucha wa Jumamosi kuamkia Jumapili nje ya mlango wa gesti akidai anamsubiri mkewe, Mama Sarah aliyekuwa na mwanaume ndani ya gesti hiyo.

Hata hivyo, Jumapili, mpaka wahudumu wanafanya usafi kwenye vyumba, mama Sarah hakuwemo ndani na mwanaume huyo aliporudi nyumbani kwake alimkuta mkewe amerudi muda si mrefu.

STEVE NYERERE AKWIDWA
Mchekeshaji maarufu hapa nchini, Steve Mangere ‘Steve Nyerere’, Ijumaa Kuu ilikuwa mbaya kwake baada ya mabaunsa wa Bendi ya Extra Bongo kumkwida na kutaka kumtesa kufuatia kumtuhumu kutaka kuingia bure kwenye onesho la bendi hiyo.

Tukio hilo lilijiri Aprili 22, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Meeda Bar, Sinza ambapo bendi hiyo ilikuwa ikimwaga burudani.
Katika tukio hilo, Steve Nyerere aliyekuwa na msanii mwingine, Salum Mchoma maarufu kama Chiki wakiwa na marafiki zao wawili walifika mlangoni na kutaka kuingia bure, tabia ambayo imeota mizizi kwa masupastaa wa Bongo.

Baada ya wasanii hao kutakiwa kutoa kiingilio, Steve Nyerere alizama mfukoni kwa hasira na kutoa Shilingi za Kibongo 20,000 na kulipa kiingilio cha watu wanne.

Wakati wakiingia, Steve alianza kuwashutumu watu wa getini kwa kumtoza kiingilio huku akiwakejeli kuwa, hawana lolote, kwanza yeye alifika ukumbini hapo kwa kuitwa na bosi wao, Chifu Kiumbe.
Majigambo hayo yalionekana kumkera mmoja wa walinzi wa getini ambaye alimvamia na kumkwida kabla ya kutaka kumshushia kipigo lakini wasamaria wema waliingilia kati na kumtoa nje ya ukumbi mlinzi huyo aliyekuwa mbogo.

Akizungumza na gazeti hili ukumbini hapo, Steve alisema yeye ameitwa ukumbini hapo na Chifu Kiumbe ambaye ni mdau mkubwa wa bendi hiyo lakini anamshangaa mlinzi huyo kujifanya kilimilimi.
“Ole wake wamemkamata, ningemfundisha adabu yule, hanijui mimi. Ningempa pigo moja tu takatifu mwenyewe angemkumbuka mama yake,” alisema Steve kwa kujitapa huku akihema kwa nguvu.

MREMBO AZIMIKA
Katika nderemo za Pasaka, ndani ya Ukumbi wa Mango Garden Kinondoni, Dar, mrembo mpya wa Bendi ya Akudo Impact ‘Vijana wa Masauti’ katika safu ya unenguaji, Mariam Sagwa alijikuta akidondoka stejini na kuzimika kwa dakika kadhaa baada ya kupandwa na ‘mzungu’ wakati akinengua.
Tukio hilo lilimkuta Mariam alipokuwa akionesha makeke ya kunengua kionjo cha ‘Ahamada Umelewa’ akilenga kuwapagawisha mashabiki waliokuwa wamefurika ukumbini humo.
Hata hivyo, wanenguaji wenzake walimpiga ‘tafu’ ya kusimama lakini alionekana akiyumbayumba hadi alipotolewa stejini.

FAGASON ABAMBWA
The Big Rapa ndani ya Bendi ya Extra Bongo, Saulo John ‘Fagason’, amejikuta akikosa uhuru alipobananishwa na mchumba wake, Angel Bushuke bila kujali kuwa mzee alikuwa mzigoni.

Tukio hilo lilichukuwa nafasi Ijumaa iliyopita saa tisa usiku katika Ukumbi wa Maeda Sinza Mori, ambapo Bendi ya Extra Bongo ilikuwa ikifanya vitu vyake.
Awali, Fagason alionekana akiinuka kila alipotakiwa kuingia katika nafasi yake ya uimbaji lakini alipomaliza tu kuimba, alilazimika kuelekea pale alipokuwa amekaa mpenzi wake kwani mama alikuwa akimsindikiza kwa macho hatua kwa hatua na kufikia mikao ya ‘kimalavidavi’.

“Mi naona ni haki yake kunibana hivi, kwa sababu ananipenda na mimi nampenda. Pia siku si nyingi tunatarajia kufunga ndoa,” alisema Fagason.

MCHUMBA WA MTU AKUTWA ‘AKIDENDEKA’ HADHARANI
Katika matukio machafu yaliyojiri ndani ya kipindi cha shamrashamra za Pasaka, ‘janki’ mmoja anayechipukia katika ulingo wa filamu za Bongo, Tabasamu Mohamed amekutwa akifanya madudu hadharani na mchumba wa mtu aliyejulikana kwa jina moja la Vumilia kwa kile kilichoonesha kuwa, alikuwa akisaka umaarufu.

Tukio hilo lilinaswa laivu na paparazi wetu Jumamosi iliyopita katika Viwanja vya Leaders Kinondoni, Dar huku watu wakiwa katika hekaheka za Sikukuu ya Pasaka.

“Siyo kama nimelewa kiviile, ila huyu ni wa kuzugia japo najua ana mchumba wake na mimi pia nina wangu,” alisema Tabasamu.

0 comments: