Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, ACP Robert Boaz.
Na Haruni Sanchawa
Watu ambao idadi yao haijafahamika jana wamefukiwa katika machimbo ya dhahabu yaliyopo katika Kijiji cha Sungu, Tarafa ya Kyabakari, mkoani Mara wakiwa kazini.
Habari zilizolifikia gazeti hili jana kabla ya kwenda mtamboni zinasema kuwa eneo ambalo kumetokea tukio hilo kumetajwa kwa jina la machimbo ya Manyaryoba yaliyoko katika Tarafa ya Kyabakari.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, ACP Robart Boaz amethibitisha kutoka kwa tukio hilo na kueleza kuwa mpaka sasa amepewa jina la mtu mmoja Bahi Obaki Yohana (30) mwenyeji wa Wilaya ya Rorya kuwa ni muongoni mwa waliofukiwa na tayari mwili wake umepelekwa Kijiji cha Marasibora kwa maziko.
Wakati huo huo, basi moja limegongana na basi dogo aina ya Coaster Kizota, mjini Dodoma na kuua watu wawili na 20 kujeruhiwa. Kamanda wa polisi wa mkoa huo hakupatikana kuzungumzia ajali hiyo.

0 comments:
Post a Comment