Social Icons

Saturday, March 26, 2011

UVAMIZI WA MAJESHI YA NATO NCHINI LIBYA WAISLAMU WAANDAMA


Watoto wenye asili ya Libya wakionyesha bango lenye maandishi Obama muuaji.

Uvamizi unaofanywa na Umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi ‘NATO’ nchini Libya umewakasirisha jumuiya ya kiislamu Tanzania ambapo waislamu wa hapa nchini walifanya maandamano ya amani siku ya jana na kufikia kilele katika viwanja vya Biafra Kinondoni jijini Dar na kupokelewa na Mufti mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Shaban Bin Simba.

Akizungumza na umati wa Waislamu waliokuwepo viwanjani hapo Mufti Simba alisema kuwa Waislamu wa Tanzania wanaungana na Waislamu wengine kote duniani, kupinga uvamizi huo ambao ni wakidhuluma kwa dini ya Kiislamu na Waislamu wote hivyo kwa niaba ya Waislamu wa nchini Tanzania anapinga uvamizi huo unaofanywa na majeshi ya ‘NATO’ kwani si haki na hiyo inaonyesha ni njia mojawapo ya kuusambaratisha Uislamu katika dunia.

Naye mwakilishi wa Ubalozi wa Libya nchini Tanzania amesema kuwa anaishukuru serikali ya Tanzania kuruhusu maandamano hayo kufanyika vile vile ameongeza kuwa anawakikishia Waislamu kuwa haki lazima itendeke kwani vita vilivyopo sasa ni kuusambaratisha Uislamu duniani na sio kuzua majeshi ya Kiongozi wa Libya Kanal Muammar Gaddafi kurusha ndege kwenye anga yao.
Mwakilishi wa ubalozi wa Libya nchini Tanzania akitoa hotuba yake.
Mufti wa Tanzania Sheikh Issa Shaban bin Simba akielezea msimamo wa Waislamu kuhusu mashambulizi yanayofanywa nchini Libya hivi sasa.
Umati wa Waislamu waliokuwepo katika viwanja vya Biafra jana kwenye maandamano hayo.

Moja ya bango likiwa limenyanyuliwa juu kwa ajili ya watu wasome ujumbe ulioandikwa kwenye bango hilo

0 comments: