Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akizungumza jambo na Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli (kushoto) wakati alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa masuala mbalimbali ya wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Rais aliitembelea wizara hiyo ikiwa ni sehemu ya utaratibu aliojiwekea wa kuzitembelea wizara, idara na taasisi mbalimbali.
Rais Kikwete (katikati) akizungumza jambo na Waziri wa Ujenzi, Dkt.John Magufuli (wa pili kutoka kushoto) na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kutoka kulia) mara baada ya kukamilisha ziara yake katika wizara ya ujenzi leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Aron Msigwa - Maelezo
0 comments:
Post a Comment