Social Icons

Thursday, March 24, 2011

MAKAMU WA RAIS DK BILAL ZIARANI MWANZA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal katikati, akiwapungia mkono wananchi wa kijiji cha Busisi wakati alipokuwa akiteremka kutoka kwenye kivuko cha M.V Misungwi, alipowasili katika kijiji hicho jana kwa ajili ya kuanza ziara ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo ya wananchi wa Wilaya ya Geita.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kalangalala Wilayani Geita baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa maabara ya Shule hiyo jana, ambapo aliahidi kuchangia shiliongi milioni tano kwa ajili ya kuanzisha kitengo cha mtandao wa intanet katika Shule hiyo. Makamu wa Rais yupo mkoani Mwanza kwa ziara ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kalangalala Wilayani Geita, baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa maabara ya Shule hiyo jana ambapo ameahidi kuchangia shilingi milioni tano kwa ajili ya kuanzisha kitengo cha mtandao wa intanet katika Shule hiyo. Makamu wa Rais yupo Mkoani Mwanza kwa ziara ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo.

Picha na Amour Nassor / Ofisi ya Makamu wa Rais

0 comments: