Social Icons

Wednesday, March 23, 2011

MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI MKOANI MWANZA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal na Balozi wa Japan Nchini Tanzania, Mhe. Hiroshi Nakagawa wakikata utepe kuzinduwa mradi wa maji safi na salama katika kijiji cha Ng’hungumalwa Wilayani Kwimba Mkoani Mwanza katika maadhimisho ya wiki ya maji kitaifa yaliyoadhimishwa jana mkoani Mwanza, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni maji kwa ajili ya miji kukabiliana na changamoto mbalimbali mijini. Kulia ni Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya. Jumla ya Shilingi Milioni 19 zimetumika hadi kukamilika kwa mradi huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimkabidhi kikombe Dorisia Mulashani, Mhandisi wa Wizara ya maji kwa ushiriki bora katika maadhimisho ya wiki ya maji kitaifa yaliyoadhimishwa jana mkoani Mwanza.
Picha na Amour Nassor-Ofisi ya Makamu wa Rais

0 comments: