Social Icons

Tuesday, February 15, 2011

TWANGA WALIVONG’AA SAUTI ZA BUSARA ZENJI

Baadhi ya wanamuziki wa ‘Twanga Pepeta’ wakiwa jukwaani.
BENDI ya African Stars International (Twanga Pepeta Sugu Kisima cha Burudani), juzikati ilifanya makamuzi ya nguvu katika tamasha la kimataifa la Sauti za Busara, ambalo hufanyika kila mwaka ndani ya Visiwa vya Zanzibar. Tamasha hilo hujumuisha makundi mbalimbali ya muziki kutoka nchi mbalimbali duniani.



Mkongwe wa muziki wa mwambao Bi Kidude (kushoto) akisalimiana na baadhi ya wanamuziki wa ‘Twanga Pepeta’.

Bi Kidude akionyesha nyonga yake jukwaani katika Sebene la ‘Twanga Pepeta’.

Kundi la Yaaba Funk kutoka Uingereza, likionyesha uwezo wake katika tamasha hilo.

Baadhi ya abiria wa boti iendayo Zanzibar wakiwa wameuchapa usingizi.

Mkurugenzi wa Bendi ya African Stars International, Asha Baraka (kulia), akiongea na wanenguaji wake muda mfupi kabla ya kupanda jukwaani.

Baadhi ya wanamuziki wa ‘Twanga Pepeta’ wakiingia ukumbini hapo.

‘Twanga Pepeta’ wakisubiri muda wa boti kwa safari ya kurejea Dar es Salaam.

Mwanamuziki wa Twanga Pepeta, Janeth Isinika, akiwa ndani ya boti.

Mashabiki waliofurika ukumbi wa Ngome Kongwe wakifuatilia burudani zilizokuwa hapo.

Wanamuziki waalikwa kutoka nje ya nchi wakiwajibika ukumbini hapo.

0 comments: