Hafsa akielezea kilichomtoa FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ ambapo alisema wingi wa wanamuziki ulisababisha kupanda jukwaani mara chache.
ALIYEKUWA mwanamuziki wa Bendi ya FM Academia, Hafsa Kazinja, na muasisi wa mtindo wa ‘Kibajaj’ ulioipatia umaarufu bendi ya Akudo Impact, na Chai Jaba, leo wametangazwa kujiunga na bendi ya Rufita Connection yenye makazi yake Tabata jijini Dar es Salaam.
Akiwatangaza wanamuziki hao katika hafla iliyofanyika Rufita Bar, Meneja Masoko wa bendi hiyo, Juma Abajalo, amesema Chai Jaba, ndiyo Rais mpya wa bendi hiyo na Hafsa atakuwa Naibu wake.
0 comments:
Post a Comment