Rais Jakaya Kikwete akikagua mahindi yanayouzwa katika soko la kimataifa la mazao la Kibaigwa wilayani Kongwa, mkoa wa Dodoma leo asubuhi wakati aliposimama kwa muda sokoni hapo kukagua na kujionea hali halisi ya upatikanaji wa mazao na uhifadhi wa mazao sokoni hapo. Kwa mujibu wa uongozi wa soko hilo, katika kipindi cha miaka sita kuanzia 2004 hadi 2010 soko hili limeweza kupokea tani za mazao 532,854 na kusafirisha tani 529,143 za mazao tofauti.
Wednesday, February 16, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment