Social Icons

Wednesday, February 2, 2011

"DEMU" AICHENGUA MIDUME KWA KUKONTRO MPIRAMSICHANA mmoja, Azile Charles, mkazi wa mkoani Morogoro, jana jioni alisababisha mchezo wa robo fainali ya

MSICHANA mmoja, Azile Charles, mkazi wa mkoani Morogoro, jana jioni alisababisha mchezo wa robo fainali ya ligi ya kugombea jezi kati ya timu ya Home Boys na Terminal iliyokuwa ikipigwa Uwanja wa Saba Saba, mjini hapa, kukosa msisimko kufuatia msichana huyo kuwateka mashabiki waliofurika katika mchezo huo uliozikutanisha timu hizo zenye upinzani mkali.
Wakati timu hizo zilipokwenda mapumziko, mashabiki hao walimuomba demu huyo anayefahamika zaidi kwa jina la Gaucho kuwaonyesha umahiri wake wa ‘kukontroli’ soka ambapo aliingia katikatika ya uwanja huo na kuanza kuuchezea mpira atakavyo ikiwa ni pamoja na kufanya hivyo akiwa amekaa chini.

Akizungumza na mtandao huu, Gaucho (jina la mcheza soka mahiri wa Brazil, Ronaldinho Gaúcho) huyo wa ‘Mji Kasoro Bahari’ alidai ana uwezo mkubwa wa kusakata soka lakini amekosa vifaa vya kufanyia mazoezi na kukosa nafasi ya kuonekana kwa wapenda soka.
Mara baada ya mwamuzi wa mchezo huo kupuliza kipenga cha kuanza ngwe ya pili ya mchezo huo, uliozikutanisha Terminal inayomilikiwa na wapiga debe wa stendi kuu ya mabasi ya Msamvu na Home Boys inayomilikiwa na wauza samaki wa soko la Mji Mpya, mashabiki lukuki waliolipa kiingilio kwenye mchezo huo walisikika wakidai walivutiwa zaidi na shoo ya demu huyo kuliko mchezo huo wa robo fainali uliozikutanisha timu hizo pinzani ambapo kila timu ilionyesha jeuri ya fedha kwa kukodi wachezaji wenye majina mkubwa ndani na nje ya mkoa wa Morogoro.

ZIFUATAZO NI PICHA ZA TUKIO HILO:

1 comments:

Anonymous said...

Kaka naomba unisaidie contacts za huyu dada ama kama unavideo ya hizi picha. naomba tuwasiliane kwa barua pepe hii, fmwemezi@yahoo.com