Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mheshimiwa Freeman Mbowe (kushoto) akiongoza Wabunge wa Chadema kutoka ndani ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma. Kulia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mheshimiwa Zitto Kabwe.
Jioni ya Tarehe 8-2-2011 kambi ya upinzani ya Chama Cha Chadema ikiongozwa na kiongozi wao, Mheshimiwa Freeman Mbowe walitoka ndani ya ukumbi wa bunge wakati kikao kikiendelea chini ya spika Anne Makinda kwa Madai ya kupinga kupitishwa kwa mabadiliko ya Kanuni za Bunge juu ya tafsiri rasmi ya KAMBI YA UPINZANI Bungeni.
Wabunge wa Chadema Wakitoka Ndani ya Ukumbi wa Bunge Jana Jioni.
0 comments:
Post a Comment