Baadhi ya viongozi wa CCM wakifuatilia kwa makini burudani iliyokuwa ikiporomoshwa na kundi la Mwaluvistanyo ambao ni muungano wa majina matano: Mwansiti, Luiza Mbutu, Vicky Kamata, Stara Thomas na Nyota Abdallah ambaye zamani alikuwa akijulikana kwa jina la Nyota Waziri.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) jana kilizindua sherehe zake za kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwake miaka 34 iliyiopita. Hafla hiyo ilifanyika viwanja vya Biafra, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Rais Mstaafu wa Zanzibar na ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Visiwani, Dk. Amani Abeid Karume, ambapo pia sherehe hizo ziliambatana na utoaji vyeti vya shukhrani kwa wale waliochangia na kufanikisha chama kushinda katika uchaguzi mkuu.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Yusuph Makamba (kushoto), akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa.
Khadija Kopa akitazama kwa makini jinsi Mwaluvistanyo (hawako pichani) wakishambulia jukwaa.
Dk. Amani Abeid Karume akimkabidhi mmoja wa wafadhili wakubwa wa CCCM waliofanikisha ushindi wa chama hicho, Moses Valentino Katabaro, ambaye ni Mwenyekiti wa Moses Foundation Tanzania.
Baadhi ya wasanii wa Mwaluvistanyo wakishambulia jukwaa wakiwa na msanii Dokii (katikati) ambaye aliungana nao.
Nyota Abdallah akiwa katika pozi jukwaani.
0 comments:
Post a Comment