Social Icons

Wednesday, January 26, 2011

WAZIRI AKERWA NA MADANGURO SHULENI



NAIBU waziri wa Ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi,Goodluck Ole Medeye amekerwa na wingi wa madanguro na vibanda vya kuonyesha picha za ngono vilivyoizunguka shule ya sekondari Enaboishu.

Ameuagiza uongozi wa kijiji , kuhakikisha kuwa ndani ya wiki moja wanaondoa madanguro,vijana wanaovuta madawa ya kulevya na vibanda vya kuonyesha picha za ngono,haraka iwezekanavyo kwani vibanda hivyo vinachangia wanafunzi wa shule hiyo kushindwa kuingia madarasani na kuishia kwenye vibanda hivyo .

Ole Medeye ambaye alikuwa mgeni rasmi, katika mahafali ya 12 ya kumaliza kidato cha 6 yaliyofanyika katika shule hiyo , mbali na agizo hilo alimtaka mkuu wa shule hiyo,Lession Ole Saking'oi kudhibiti nidhamu na kuhakikisha wanafunzi hao hawashiriki vitendo vichafu shuleni hapo.

Naibu waziri huyo alishtushwa na taarifa hiyo baada ya kuisikia katika risala iliyosomwa na wanafunzi wa shule hiyo , ikibainisha kwamba, vibanda hivyo vya ngono vimekuwa kero na vimechangia kwa kiasi kikubwa kuporomoka kwa maadili kwa wanafunzi wa shule hiyo ,kutokana na mambo mbalimbali ikiwemo ukosefu wa uzio unaozunguka eneo la shule.

Mmoja wa wanafunzi hao ambaye ni kiongozi wa wanafunzi hao ,Shangwe Alex alimwambia mgeni rasmi kuwa amelazimika yeye na wenzake kuushauri uongozi wa shule hiyo wakipendekeza, wanafunzi wa kike wabadili mavazi yao badala ya kuvaa sketi na shati pekee ,wawe wanavaa suruwali ndani ya sketi.

Alex alisema kuwa hali hiyo baada ya uongozi kutafakari na kukubali imesaidia kwa kiasi kikubwa kurudisha heshina na nidhamu kwa wanafunzi wa kike .

Awali wawanafunzi wa kike walikuwa wakivaa sketi fupi kupita kiasi na kuacha sehemu kubwa ya maungo yao wazi, kutokana na kujihusisha zaidi na kuangalia picha za utupu na kujikuta wakishawishika kufanya ngono na wanafunzi wenzao wa kiume na vijana wanaoishi jirani na eneo hilo na kusahau wajibu wao wa kusoma.

Aidha kwa upande wa mkuu wa shule hiyo,Mwalimu Saking'oi pamoja na kukiri kuwepo kwa vibanda hivyo vya ngono,ameahidi kushirikiana na uongozi wa eneo hilo kuhakikisha vinaondolewa haraka iwezekenavyo.

Katika mahafali hayo jumla ya wanafunzi 128 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya kidato cha sita katika shule hiyo.

0 comments: