Social Icons

Thursday, January 13, 2011

NAIBU WAZIRI WIZARA YA UCHUKUZI APOKEA MISAADA KUTOKA CHINA

Naibu Waziri Wizara ya Uchukuzi, Dk. Athuman Mfutakamba ambaye ni Mbunge Jimbo la Igalula Mkoani, Tabora akijaribu Moja kati ya baiskeli 20 alizokabidhiwa kama msaada na Balozi wa China, Nchini Tanzania, Liu Xianshen (kulia) kwa ajili ya Wananchi wa Jimbo la Igalula Mkoani Tabora, makabidhiano hayo yalifanyika jana kwenye ubalozi wa China, nchini Tanzania.

Mheshimiwa Dk. Mfutakamba (kushoto) akiangalia baiskeli pamoja na balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xianshen mara baada ya makabidhiano hayo.
Dk. Mfutakamba (kushoto) akijaribu cherehani moja kati ya 20, kulia kwake ni balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xianshen.


Picha kwa hisani ya Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano - Wizara ya Miundombinu.

0 comments: