Social Icons

Monday, January 3, 2011

MACHOZI, VICHEKO MKESHA WA MWAKA MPYA MORO‏

Baadhi ya waumini wa kanisa la KKKT Usharika wa Mji Mpya mjini Morogoro, wakilia baada ya kengele ya kanisa hilo kupigwa majira ya saa sita kamili ikiwa ishara ya kuupokea mwaka 2011.

MKESHA wa ibada ya kuuaga mwaka 2010 na kuukaribisha 2011 iliyofanyika Desemba 31 kuanzia majira ya saa tatu usiku hadi saa sita ndani ya kanisa la KKKT Usharika wa Mji Mpya mjini Morogoro, ulikuwa wa aina yake ambapo baadhi ya waumini baada ya kuingia mwaka mpya waliangua vilio wengine wakiangusha vicheko.

Pichani ni baadhi ya waumini wakiangua vilio na wale waliokuwa wakifurahia tukio hilo baada ya kengele ya kanisa hilo kupigwa majira ya saa sita kamili ikiwa ishara ya kuupokea mwaka 2011.

Mtandao huu ambao ulikuwemo ndani ya kanisa hilo mwanzo mpaka mwisho wa ibada hiyo,ulifanikiwa kuzungumza na waumini hao ambapo walidai kwamba walishindwa kujizuia baada ya kukumbuka matukio mengi ya mwaka uliopita.

"Binafsi nilishindwa kujizuia baada ya kuvuka mwaka uliopita ambapo nilikumbuka matukio mengi yaliyopita yakiwemo kupoteza wapendwa wangu. Lakini zaidi ya yote ni mambo makubwa aliyonifanyia Muumba wangu. Sina cha kumlipa zaidi ya kumshukuru na kuomba damu ya Yesu izidi kunifunika mwaka huu mpya," alisema muumni mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Pendo.


0 comments: