Jerry Muro akitoka mahakamani leo asubuhi baada ya kesi kuahirishwa.
KESI ya kutaka kupokea rushwa ya shilingi milioni kumi inayomkabili aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha runinga cha taifa, TBC1, Jerry Muro, na wenzake katika mahakama ya Kisutu jijini Dar, imekwama kusikilizwa baada ya upande wa mashitaka kushindwa kumfikisha shahidi wake mahakamani hapo. Sababu nyingine iliyokwamisha kesi hiyo ni wakili wa utetezi, Majura Magafu, ambaye aliomba udhuru baada kupatwa na msiba.
0 comments:
Post a Comment