Social Icons

Tuesday, January 4, 2011

KABURI LA KIYEYEU LAHAMISHWA

Fuvu la Kiyeyeu aliyekuwa Mganga wa Jadi, mkazi wa kijiji cha Mlolo, Kata ya Mseke Wilaya ya Iringa Vijijini baada ya kufukuliwa na kutolewa kaburini.

KUMEKUWA na matukio ya ajabu na ya kutisha yaliyokuwa yakitokea katika kabiri hilo la aliyewahi kuwa Mganga maarufu wa Jadi Mkoani Iringa kugoma kuhama katika eneo ililopo.Mara kadhaa kaburi hilo limekuwa likijaribu kuhamishwa kutokana na kuwa zaidi eneo la karibu na barabara lakini hutokea maajabu ambayo hutisha watendaji wa kazi hiyo na kuamua kuliacha kama lilivyo.Aidha tukio la kwanza ni lile la watu wa Tanesco walipojaribu kutaka kulihamisha kaburi hili ili kuweza kupitisha nguzo za umeme eneo hilo, lakini kaburi hilo lilionyesha dalili za kutotaka kuhama wala kuvunjika.Baada ya kushindwa kuhamisha kaburi hilo, wahusika waliamua kupitisha nyaya za umeme bila kuliondoa, lakini nyaya hizo zilishindwa kupitisha umeme kutoka mwanzo wa kaburi hilo hadi mwisho wa kaburi hilo yaani kwa jinsi zilivyokuwa zimefungwa kupitia juu ya kaburi hilo.Kufuatia tukio hilo, wahusika iliwalazimu kukwepa eneo hilo la juu ya kaburi kwa kuhamisha nyaya na kuhamishia upande wa pili wa barara hadi walipolivuka kaburi hilo na ndipo umeme ukakubari kuwaka hadi leo.Lakini cha kushangaza ni tukio la sasa hivi ambapo eneo hilo linatanuliwa kwa ajili ya upanuzi wa barabara na wahusika wamefanikiwa kulihamisha kaburi hilo kiulaini kabisa ili kupisha upanuzi huo. Sasa sijui kama itatokea maajabu mengine huko litakapohamishiwa ama la wote tusubiri kusikia.
Mabaki ya mwili wa Kiyeyeu yakiwekwa katika jeneza tayari kwa kwenda kuzikwa upya baada ya eneo la awali kuvunjwa ili kupisha upanuzi wa barabara kuu ya Iringa –Mbeya.Jumla ya makaburi nane yameondolewa katika eneo hilo na hakuna tukio lolote la ajabu lililojitokeza pamoja na kuwapo kwa dalili za woga.

Picha Zote na Francis Godwin, Iringa

0 comments: