Social Icons

Tuesday, January 4, 2011

JE, UNAFIKIRI NINI KUHUSIANA NA HILI SUALA?


KWANINI watu wamezama sana kwenye burdani siku hizi, je unafikiri nini kuhusiana na hili swala? behind of the scene kuna jambo kubwa sana limejificha, wape starehe wajisahau waibie. Hili liliwakuta ndugu zetu kule Zaire enzi za Mabutu na sasa lipo hapa nyumbani, Watanzania hawajafikia uchumi wa nchi za magharibi ambapo mtu anaweza kuishi bila wasiwasi hata kama hafanyi kazi kwa maisha yake yote, na kila unapokuwa na familia kumbwa ndio maisha yako yanakuwa mazuri, utalipwa hela nyingi na kupatiwa nyumba kubwa zaidi. huhitajiki kufanya kazi. yote haya yalipatikana kwa kuiba kutoka nchi zetu changa na kupeleka uchumi wetu kwao.
Kwa kuwa baada ya uhuru unawawia vigumu kuiba kati scale ile kabla ya uhuru sasa wanakuja na staili nyengine ili kuwafanya raia wao kuishi maisha yale yale waliyozoea, hasa baada yauchumi wao na dunia kuharibika, wajitahidi kuja na mtindo wa investiment huku wakuchukua pesa kwa njia ya hisa, ili wakubane na wewe wanaweka starehe ili wewe waliyekutuma uwafanyie kazi yao uendelee kulipia kile kidogo eti unajiburudisha ili nacho wakichukue, hebu chuku mfano wewe unafanya kazi kati benki mojawapo hapo mjini mbayo inamilikiwa na hao tuliokuwa tunawaita wakoloni, wakisha kulipa mshahara wako wanugawa kati mafungu mbalimbali, mahitaji muhimu na yasio muhimu, chukulia wewe ni kujibajeti 50%/50%.
Ikifika weekend unajifanya unatoka na familia au rafiki zako kwenda kutumia, utaagiza chakula na vinywaji, wamiliki wa kampuni za vinywaji ni hao wakoloni na sasa wao wanaagiza chakula wanachokupikia toka kwao wewe unanunua kwa bei mbaya mwisho wa mwezi nusu au zaidi yamshara wako inakwenda kwao.
Je nani hapo ataendelea kuwa na maisha mazuri? vitu vingi tunavyonunua havitoki nchini kwetu je nani anatajirika, jiulize kuanzia leo kwanini wewe Mtanzania usitumie hizo pesa za ziada kuwekeza nchini kwako kama vile kilimo au ujenzi wa nyumba ukawapangisha hao wanajiita investors?
weka akiba na earn interest uone kama wataendelea kuwekeza kama wakiona hawapati kile wanachotaka, sisemi kuwa usiende kwenye starehe, jaribu sana kuangalia starehe ipi inakunufasha wewe kama Mtanzania na sio hao wengine.
Tusibweteke na starehe tunazozifanya hivi sasa tunatakiwa tufikiri sana kuhusu mustakabali wa maisha yetu sasa na vizazi vyetu baadae, Ndio maana hivi sasa watu wanashindana kuiba toka serikalini na kwengine ili kuwa nakiwango kikubwa cha akiba nje ya nchi. ndio maana watu hivi sasa wanadai madai ya katiba mpya, hili litasaidia katika uchumi wetu na sio tu kwenye siasa.
Wakoloni baada ya research ya muda mrefu wamekuja na falsafa mpya - ukitaka kumwibia Mwafrika mpe starehe, ukitaka kumuibia Mwarabu - mtishe, Ukitaka kumwibia Muhindi - invest katika sekta ya mawasiliano na sio heavy industry maana atacopy na kuanzisha yake nawe utabaki huna kitu, ukitaka kumuibia muasia kama vile Mchina Mkorea na Mjapani - Invest katika viwanda na wagomanishe ukijifanya unawalinda lakini hili walikosea kwa Mchina na wanajuta hivi sasa lakini walipatia kwa Korea na Japani.
Ndugu zangu Watanzania umefika wakati Tunatakiwa tufikirie mara mbili badala ya kujiingiza katiaka starehe kama hizo za kamari (Casino) nani anafaidika? kwanini baadhi ya watu nchini Marekani na Ulaya wamepigwa marufuku kucheza kamari?
Umefika wakati tusikubali kuibiwa kwa starehe hewa ukiamka huna kitu, mna elimu yakutosha kupambua lipi baya na zuri, wekezeni katika nchi yenu na saidianeni mafanikio yatapatikana, Ni matumaini yangu Mhariri utayapokea na kuwafikishia Watanzania wenzangu kuhusu hili, nitaendelea kuandika makala haya kwa urefu pindi ukinipa nafasi japo mara moja kwa mwezi katika makala maalumu.

(Na Msomaji wa mtandao)

0 comments: