Washindi wa tuzo za Filamucentral bora za 2010 wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi na waratibu wa tuzo hizo kwenye hafla fupi iliyofanyika hoteli ya Tamal, Mwenge jijini Dar es Salaam leo.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Prof. Martin Mhando akimkabidhi cheti cha Muigizaji bora wa Filamu pamoja na cheti cha Mtayarishaji bora wa Filamu 2010, Steven Kanumba.
Mwakilishi wa ZIFF, Bw. Daniel Nyarusi akimkabidhi vyeti muigizaji mahiri wa filamu nchini Ray Kigosi. Ray amejinyakulia tuzo, vyeti vitatu ambavyo ni tuzo ya utengenezaji bora wa 'cover' za filamu, muongozaji bora wa filamu na utengenezaji bora wa filamu wa kampuni yake.
Mgeni rasmi, ambaye pia ni Mkurugenzi ZIFF, Prof Martin Mhando akimkabidhi tuzo yake Jenifer Daudi ya Muigizaji bora chipukizi wa filamu 2010, Jenifer ameibuka na tuzo hiyo mara baada ya kuonyesha umahiri mkubwa katika uigizaji kupitia filamu ya This is it pamoja na Uncle JJ za Kanumba. Hafla hii imefanyika mapema leo mchana ndani ya hotel ya Tamal, Mwenge jijini Dar.
0 comments:
Post a Comment