Mwenyekiti wa Twanga Pepeta, Baraka Msilwa (wa tatu kushoto), akiongoza safu ya wafungua ‘Shampeni’.
BENDI ya African Stars International (Twanga Pepeta Sugu Kisima cha Burudani) usiku wa kuamkia leo walimwaga burudani kali iliyokwenda sambamba na pati yao iliyojulikana kwa jina la Celebrity Party ndani ya ukumbi wa Mzalendo Pub ulioko Millennium Tower, Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.
Shughuli hiyo iliyoshirikisha mastaa kutoka tasnia mbalimbali hapa nchini ilihudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Mh. Iddi Azzan akiwa mgeni rasmi.
Mwenyekiti wa Twanga Pepeta, Baraka Msilwa, akiongea jambo katika hafla hiyo.
Mh. Idd Azzan (kulia), akimlisha ndafu mkurugenzi wa bendi hiyo, Asha Baraka.
Mchekeshaji wa kundi la Orijino Komedi, Emmanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji), akichukua mlo kwenye hafla hiyo.
Baadhi ya wasanii waalikwa wakibadilishana mawazo ukumbini hapo.
Waimbaji wa bendi hiyo wakiwajibika jukwaani.
I
dd Azzan (katikati), akitoa ‘mawili-matatu’ katika hafla hiyo.
Baraka Msilwa (katikati), akigongeshana ‘cheers’ na wageni waalikwa.
Mwimbaji wa zamani wa bendi hiyo, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ (kushoto), akibadilishana mawazo na msanii wa filamu nchini Mahsen Awadhi ‘Dk. Cheni’
0 comments:
Post a Comment