Social Icons

Thursday, December 9, 2010

WATANZANIA WAADHIMISHA MIAKA 49 YA UHURU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akielekea kukagua gwaride la maadhimisho ya sherehe za Uhuru zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam

WATANZANIA kwa ujumla wao, wanajivunia uhuru kwa kuadhimisha kutimiza miaka 49 tangu Tanganyika kuzaliwa kwake Desemba 9 mwaka 1961, ambapo leo kulikuwa na sherehe za maadhimisho hayo ambayo yamefanyika kitaifa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete huku wageni mbalimbali wa kitaifa na kimataifa wakiwa wamealikwa.
Katika maadhimisho hayo, Rais Kikwete, alikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama ambavyo ni Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).


Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania, Augustino Nanyaro akiwa amesimama na Mkuu wa gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama wakisubiri kupokea viongozi mbalimbali wa serikali.


Kamamda wa Kanda maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova, akiwekwa sawa na mlinzi wake tayari kwa kupokea wageni waalikwa.


Mkuu wa Jeshi la Polisi, Said Mwema (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania, Augustino Nanyaro mara baada ya kuwasili uwanjani hapo.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda, akiwasili kuungana na wageni waalikwa kwenye sherehe hiyo.


Wake wa Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal wakiwasili uwanjani hapo kama wanavyonekana pichani.

0 comments: