Social Icons

Monday, December 13, 2010

STARS WALAMBA KITITA ATRIUMS HOTEL

Meneja wa Hotel yaThe Atriums, Hudgson Wilson (kulia) akimkabidhi kitita cha shilingi milioni mbili Nahodha wa Kilimanjaro Stars, Shadrack Nsajigwa. Makabidhiano hayo yamefanyika asubuhi leo hotelini hapo, Sinza Africa Sana jijini Dar es salaam


Meneja wa hotel akiongea machache na wachezaji wa Kilimanjaro stars kabla ya kukabidhi fedha hizo

Wachezaji na Kocha Mkuu, Jan Poulsen, Sylvester Marsh (kushoto0 wakisikiliza maelezo ya meneja huyo

Mkurugenzi wa Zizzou fashion, Tippo Athumani (aliyeshika kombe) akiwa katika picha ya pamoja na makocha wa Timu ya Taifa, Sylvester Marsh (kulia) Pousen na daktari wa timu.

Mchezaji mahiri wa Taifa Stars, Mrisho Ngassa (aliyeshika kombe), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wake pamoja na wadau wa soka waliokuwepo hotelini hapo

Ngasa akiwa na makocha wake Marsh na Paoulsen.


HOTELI ya Kisasa ya The Atriums iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam, leo imewajaza wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars mamilioni ya shilingi kutokana na kutoa ubingwa wa Chalenji.
Stars imekuwa ikiweka kambi yake kwenye hoteli hiyo iliyopo maeneo ya Sinza Afrika Sana kila inapojiandaa na michuano ya kimataifa au ya kirafiki.
Akizungumza na Championi, Meneja wa The Atriums Hudgson Wilson, alisema kuwa wameamua kutoa motisha hiyo kwa wachezaji wa Stars kwa kuwa wamekuwa nao kwa muda mrefu.
“Sisi kama menejimenti ya hoteli tumeamua kuwapa motisha vijana wetu baada ya kufanikiwa kuchukua ubingwa wa Kombe la Chalenji.
“Tumekaa na kuona kuwa hawa ni wateja wetu wazuri, na kwa kuwa wameonyesha mwanga kwa kulipa heshima taifa, uongozi chini ya Mkurugenzi wetu Eric Shigongo umeamua kutoa kitita cha shilingi milioni mbili (2,000,000), kwa wachezaji hao ambao tumekuwa tukiishi nao mara kwa mara,” alisema meneja huyo.
Stars imekuwa ikiweka kambi ndani ya hoteli hiyo mara kwa mara na wachezaji wa timu hiyo wamekuwa wakiisifu kutokana na huduma zake kuwa nzuri.


0 comments: