Social Icons

Friday, November 5, 2010

SWAHILI FASHION YAZINDI KUUNGURUMA DAR

Wanamitindo wakipita jukwaani.

WANAMITINDO mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania, jana usiku walionesha ubunifu wao wa mavazi katika onesho lililofanyika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yanayoendelea viwanjani hapo mpaka kesho Jumamosi, yameandaliwa na mbunifu maarufu hapa nchini, Mustapha Hassanally.


Wadau wa mitindo, Martin Kadinda (kushoto) na Jenny Hemed, wakifuatilia onesho hilo.


Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Ghonche Materego akiwa eneo la tukio.


Mwanamitindo, Fideline Iranga (kulia) na shosti wake aitwae Warda, nao wakionesha vivazi vyao mbele ya kamera ya paparazzi wetu.


Mwanamitindo, Hadija Mwanamboka (kulia), akiteta jambo na mdau mmoja wa fani hiyo wakati onesho likiendelea.


Fideline katika pozi.


Kwa mujibu wa watayarishaji wa onesho hilo, vivazi hivi ni maalum kwa ajili ya kujikinga na malaria.


Akiwa katika vazi la kujikinga na malaria, mwanamitindo huyu anaonesha jinsi mtoto anavyoweza kukingwa na malaria kwa kubebwa kwenye chandarua maalum.


0 comments: