Mrisho Mpoto aka Mjomba akisisitiza jambo wakati akiwasilisha mada yake kwenye Jukwaa la Sanaa Jumatatu
hii.Aliwashauri wasanii wa Bongo kutokuwa malimbukeni wa sanaa za nje na kuacha asili zao.
Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yaliyojitokeza kwenye
Jukwaa la Sanaa.Aliendelea kutoa wito kwa wasanii kujikita kwenye sanaa za asili na kuacha kunakiri kazi za nje
kwani hakutawasaidia kitu.
Wasanii wakichangia mada kwenye Jukwaa la Sanaa.
wao kwenye tasnia ya sanaa na kubeba zaidi sanaa ya asili yenye utambulisho wa Tanzania.
Wengi walitoa wito kwa wasanii kubadili muenendo
Mjomba akiongea kwa uchungu juu ya tabia ya wasanii wa Bongo kukopi miziki ya nje na kufanya sanaa
isiyokuwa na asili yao.
MSANII mahiri wa mashairi nchini,Mrisho Mpoto ameeleza kile anachoamini kwamba,tasnia ya sanaa na wasanii wa
Bongo hawawezi kamwe kupata mafanikio katika ngazi ya kimataifa kutokana na ulimbukeni wa kuiga sanaa za
watu wengine, kudharau asili yao na kujipachika usupastaa wa kubumba.
Mpoto aliyasema hayo wakati akiwasilisha mada yake iliyohusu Muziki wa Asili na Mashairi kwenye Jukwaa la
Sanaa Jumatatu hii ambapo alisisitiza kwamba,wasanii wa bongo wamekuwa ni wa kulalama na kulia njaa
kutokana na kazi wanazozalisha kushindwa kabisa kupata mvuto wa kimataifa na kushindana kwani zimekuwa kwa
asilimia kubwa zikifanana na tamaduni za nje hivyo kukosa jipya.
Akijitolea mfano yeye mwenyewe Mpoto alisema kwamba, ameweza kukaa chini na kubuni sanaa ya asili ya
Tanzania ambapo amekuwa akighani mashairi na kuyaweka kwenye mdundo wa muziki na hivyo kupendwa na
idadi kubwa ya watanzania na kupenya kimataifa hivyo kumfanya kupata mialiko na fursa nyingi za fedha ambazo
zimekuwa zikimpatia mafanikio makubwa.
Kwake yeye Mpoto anaamini kwamba, Sanaa ya Tanzania na wasanii wake hawaonekani kugundua siri ya kufanya
kazi za sanaa zenye asili yao na badala yake wamekuwa makasuku wa kujifananisha na kuishi maisha kama ya
Ulaya na Marekani huku kazi zao zikifanana kila kitu na hizo za nje hali ambayo imeifanya sanaa kupwaya na
wasanii wenyewe kuishi maisha ya njaa.
Aliongeza kwamba, ni ngumu kupata msanii wa bongo anayefanya sanaa peke yake kwani mara nyingi lazima
wachanganye na shughuli zingine ili kupata kipato kutokana na kazi zao kutowalipa.Katika hili Mpoto anaamini
kwa kiasi kikubwa limesababishwa na wasanii wenyewe kukosa ubunifu, kuiga kila kitu kutoka nje, kulewa sifa za
mapema, kukumbatia sanaa zisizo za asili yao na kujipachika usupastaa wa kubumba.
“Nimekuwa nikipata mialiko mingi nje ya nchi,siku chache zijazo nitaenda Denmark,Finland,Ufaransa, na
Uholanzi.Si kwa kuwa napendwa sana bali ni aina ya sanaa ninayofanya ina asili yangu ya Tanzania na
inanitambulisha kila ninakokwenda.Waache wasanii wengine wavae nguo chini ya makalio yao au hata watembee
uchi mimi nitabaki na magunia yangu.Hili ndilo naamini litaweza kunipa mafanikio na ninayapata” alisisitiza
Mpoto.Mpoto ambaye kwa sasa ni msanii pekee aliyepata mafanikio makubwa kutokana na kupata mikataba mingi ya
matangazo, mauzo ya kazi zake na mialiko ya kimataifa kutokana na kukumbatia sanaa ya asili aliwashauri wasanii
wa bongo kuacha kunakiri (kukopi) sanaa za nje na badala yake wakune vichwa katika kubeba sanaa ya asili
ambayo hapana shaka itawatambulisha kimataifa na kuwapa mikataba minono ya ndani na ya nje.
Mpoto aliyekuwa ameambatana na muimbaji wake wa Mjomba Band,Ismail alisema kwamba, inatia aibu na kinyaa
unapoangalia sanaa za bongo kwani zinaonekana kuandaliwa na watu wenye njaa, wanaosaka fedha za fastafasta
kuliko kujali nini wanapeleka sokoni hali ambayo imekuwa ikiwafanya wasanii wa Tanzania waonekane ni wa
hovyohovyo, wa kudharaulika na wasio na mkakati wa kufikia mafanikio ya kisanaa.
“Kuna watu wamefanya sanaa miaka nenda miaka rudi lakini hawapigi hatua.Wamekuwa ni watu wa kulalamika
bila kuzingatia ni kwa kiwango gani sanaa zao zina ubunifu na kubeba asili na utambulisho wao.Ndugu zangu
tusipozingatia haya mafaniko tutayasikia tu na tutakuwa watu wa kuganga njaa na kupiga mizinga ya vocha”
alimalizia Mpoto.
0 comments:
Post a Comment