John Mnyika akiwaonesha wananchi hati ya ushindi wa Ubunge Jimbo la Ubungo baada ya kutangazwa mshindi leo katika Viwanja wa Loyola.
Akitangaza matokeo hayo leo katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Loyola Mkurugenzi Lubuva alisema kwa mujibu wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi anatangaza rasmi na kumkabidhi hati maalum ya ushindi Mnyika hali iliyofanya umati wa watu waliokuwa wakishuhudia kujawa na furaha kwa kumshangilia.
Kwa upande wake mbunge huyo kijana mteule amewaahidi wapiga kura na wananchi wengine wa jimbo hilo kuwa atafanya kazi kwa uadilifu mkubwa bila kujali chama, dini wala kabila na alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wale wote waliokuwa wakisubiri matokeo hayo kutangazwa kwa uvumilivu mkubwa waliouonesha kwa siku tatu walizokesha kusubiria.
Mara baada ya kutangazwa matokeo hayo na Mnyika kutoa neno la shukurani wapenzi wa Chadema walianza kuimba na kufanya maandamano makubwa kuelekea makao makuu ya chama chao, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Mkurungenzi wa Usimamizi wa Uchaguzi Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni, John Lubuva akitangaza matokeo ya ubunge jimbo la Ubungo leo.
Mama yake John Mnyika akiwaarifu ndugu, jamaa marafiki ushindi wa John Mnyika katika nafasi ya ubunge.
Mnyika akianza maandamano kuelekea makao makuu ya chama chao baada ya kutangazwa mshindi.
Askari wa Jeshi la Polisi, kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wakifanya doria leo katika Viwanja vya Shule ya Loyola ambako matangazo ya matokeo ya ubunge Jimbo la Ubungo yalikuwa yakitangazwa
Haikuwa kazi rahisi, mashabiki wa Chadema iliwabidi kupunguza usingizi baada ya kukesha kwa siku mbili, hapa wanauchapa usingizi katika viwanja vya Loyola baada ya kucheleweshwa kutangazwa mshindi.
Mnyika: Nawashukuruni sana wote walionipa kura na hata wale walioninyima, tupo pamoja, nisingeshinda kama sio nyinyi vijana wa mitaani.
0 comments:
Post a Comment