Mpiga picha wetu usiku wa kumakia leo alikuwa katika ukumbi wa Mango Garden ambako kulikuwa na onyesho la African Stars ambao walikuwa wakitoa burudani ya kukata na shoka ikiongozwa na safu mahiri ya wanenguaji kama wanavyoonekana pichani.
Wapiga gitaa mahiri wa African Stars AdoLf Mbinga (kushoto) na Ally Akida wakipiga magitaa katika onyesho la bendi hiyo lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa nyumbani, Mango Garden.
Wanenguaji wa bendi hiyo wakimpongeza mwanamuziki wa Jahazi, Thabiti Abdul kwa upigaji wake wa Kinanda.
Mtangazaji wa kituo cha TV cha TBC1, Ben Kinyaiya akichukua namba ya simu ya mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima, Khadija Kalili.
Mtangazaji wa Redio Times Hadija Shaibu ‘Dida’ akionekana mwenye mawazo mengi.
0 comments:
Post a Comment