PENGINE ulikuwa hujui, lakini tambua sasa! Kwamba kuna mastaa kibao Bongo ambao ni ndugu lakini mashabiki wao hawajui kama ni ndugu.
Ndugu hao mastaa wanaendelea kutesa kunako fani mbalimbali huku wakijizolea umaarufu kila kukicha kutokana na vipaji vyao.
Kutokana na hali hiyo, leo tunawaletea watu hao maarufu ambao ni ndugu, lengo ni kuwajulisha wasomaji nani ni nani.
FERUZI, MLASI:
Hawa ni ndugu toka, nitoke (mtu na dada yake). Wote wanajulikana kupitia kazi zao za muziki. Mrisho Feruzi ‘Ferouz’ aliwahi kutamba na kundi la Daz Nunda na pia kwenye nyimbo mbalimbali ukiwemo ule maarufu zaidi wa Starehe (aliomshirikisha Profesa J).
Dada yake, Mlasi Feruzi yeye amevuma sana kwa wimbo wake unaowazungumzia wapendanao, Maproso akiwa na Bicco Stars.
ROSE NDAUKA, DIDA:
Undugu wa hawa ni mjomba na shangazi. Mama yake mzazi Rose na baba mzazi wa Dida (sasa marehemu) ni toka nitoke, mkubwa ni baba yake Dida. Rose ni nyota wa filamu za Kibongo, Dida au Khadija Shaibu ni mtangazaji wa Radio TIMES FM ya jijini Dar.
KANUMBA, DOTNATA:
Wote ni mastaa wa filamu. Undugu wao, mama mzazi wa Kanumba ni dada wa Dotnata, kwa hiyo Kanumba akimwona Dotnata anamwita mama mdogo.
MZEE MAGALI, SISTER FAY:
Ni baba na mwana, baada ya kumpotezea mama yake Fay kufuatia ujauzito aliompa, ndipo katika ukubwa, juzikati Charles Magali akakutana na mwanaye huyo. Baba ni staa wa filamu Bongo, mwana ni sitaa wa muziki wa Kizazi Kipya, alitamba na kibao cha Ninakataa Ugali (aliomshirikishwa na Masanja Mkandamizaji).
JACK WOLPER, SYLVIA SHALLY:
Jacqueline Wolper Masawe, yeye amepandia sanaa ya maigizo, Sylvia ametokea ulimbwende, alikuwa Miss Ilala, 2009.
Udugu wao ni mmoja anazaliwa na mdogo, mwingine na mkubwa. Yaani ni mtoto wa mama mkubwa kwa mama mdogo.
SHAMSA FORD, WABOGOJO:
Ni mtu na kaka yake, Shamsa anakuja kwa kasi kwenye filamu za Bongo, Wabogojo ni maarufu kwa mambo ya sanaa ya sarakasi, anamudu kupindisha viungo vyake vile anavyotaka, pia ni mnenguaji.
Katika kuzaliwa kwa mzee Ford (sasa marehemu), alianza Wabojo, akafuatia Shamsa.
FATMA ALMASI NYANGASA, MWASITI ALMASI:
Hawa wametoka tumbo moja, mkubwa Fatma Almasi Nyangasa. Jina la Nyangasa ni la mumewe baada ya kuolewa kwa ndoa. Yeye ni Mtangazaji wa ITV na Radio One, mdogo wake Mwasiti ni mwanamuziki mahiri wa Bongo Flava.
MASANJA MKANDAMIZAJI, AISHA WA ‘MAMBO HAYO’:
Kidogo kuna utata, lakini mtu wa uhakika amesema ni ndugu, yaani katika kuzaliwa alianza Thecla Mugaya ‘Aisha’ akafuatia Emanuel Mugaya ‘Masanja’. Wote ni wasanii wa maigizo, lakini Aisha ‘alistop’ baada ya kuolewa.
Hao ni wale ambao udugu wao haukuwa wazi sana, hata hivyo, wapo wengi ndugu na wanatamba katika fani. Mfano, wanamuziki wa Bongo Flava, Banana Ali Zorro na Maunda Ali Zorro.
Wengine ni Yvonne Cherly ‘Monalisa’ (mtoto) na Suzane Lewis ‘Natasha’ (mama) na Khadija Yusuf (dada) na Mzee Yusuf (kaka).
Pia, Omary Kopa (mtoto) sasa marehemu na Khadija Omary Kopa (mama) ambaye bado anatamba katika miondoko ya taarab.
Omary Tego (kaka) na Maua Tego (dada) wote waimbaji wa taarab katika kundi la Coast Modern Taarab.
Kama vile haitoshi, Saida Said Mwilima (dada) sasa ameolewa nje ya nchi na Sauda Said Mwilima ambaye ni Mtangazaji wa Star tv.

0 comments:
Post a Comment