MSHINDI namba nne wa mchuano wa Big Brother All Stars mwaka huu Mtanzania, Mwisho Mwampamba, leo amezawadiwa na kampuni ya Multi Choice mashine ya HD PVR itakayomwezesha kuangalia vipindi mbalimbali vya televisheni kupitia DSTV.Hafla hiyo ilifanyika mbele ya waandishi wa habari katika hoteli ya Holiday Inn jijini Dar es Salaam.
Multi Choice Tanzania ndiyo ilikuwa mdhamini wa Mtanzania huyo na ndiyo waliomwezesha kushiriki kinyang’anyiro hicho.
Katika hafla hiyo iliyosimamiwa na Meneja Masoko wa Multi Choice, Furaha Sawalu na Afisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Barbra Kambogi, Mwampamba aliwaeleza machache waandishi wa habari kuhusu mchuano huo ulivyokuwa.
Mwisho Mwampamba (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Furaha Sawalu (kushoto) na Barbra Kambogi.
Mwisho Mwampamba akisikiliza baadhi ya maswali yaliyokuwa yakiulizwa na waandishi wa habari katika hafla hiyo.
Furaha Sawalu akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.
Baadhi ya waandishi wa habari waliofika kwenye hafla hiyo wakifuatilia zoezi.
Furaha Sawalu (kushoto) akimkabidhi mashine ya HD PVR Mwisho Mwampamba ikiwa moja ya zawadi itakayomwezesha kufuatilia baadhi ya vipindi vya DSTV bure kila siku. Anayeshuhudia zoezi hilo ni Barbra Kambogi
Multi Choice Tanzania ndiyo ilikuwa mdhamini wa Mtanzania huyo na ndiyo waliomwezesha kushiriki kinyang’anyiro hicho.
Katika hafla hiyo iliyosimamiwa na Meneja Masoko wa Multi Choice, Furaha Sawalu na Afisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Barbra Kambogi, Mwampamba aliwaeleza machache waandishi wa habari kuhusu mchuano huo ulivyokuwa.
0 comments:
Post a Comment