Social Icons

Saturday, October 16, 2010

MAPACHA WATATU WAFUNIKA TRAVERTINE!!

Wasanii wanaounda kundi la Mapacha Watatu, kutoka kushoto ni Joseph Michael a.k.a Jose Mara, Khalid Chuma a.k.a Chokoraa na Kalala Junior wakifanya makamuzi jukwaani usiku wa kumakia leo.Usiku wa kuamkia leo wapenzi wa burudani walifurika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Travertine, uliopo Magomeni jijini Dar es Salaam, kushuhudia shoo ya kundi la Mapacha W3 ambayo ilinogeshwa na bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’ na bosi wa Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf. Mpango mzima ulikuwa kama picha zinavyoonesha


Mmoja wa mashabiki akimtunza Mzee Yusuf wakati akinogesha onesho hilo.

Jose Mara (kushoto) akipagawisha mashabiki.

Wasanii maarufu wa filamu za Kibongo, Shumileta (kulia) na Zamda wakiwa kwenye onesho hilo.

Mnenguaji wa ‘Twanga’ Maria Salome muda mwingi alionekana ukumbini hapo akihangaika kutafuta mawasiliano ya simu na mtu ambaye hakufahamika mara moja.

Wakati Mapacha Wa3 wakikamua ndani ya Travertine, ukumbi wa Meeda Sinza, bendi ya Diamond Musica International ‘Vijana Classic’ ilikuwa ikifanya makamuzi kama wanavyoonekana wanenguaji hawa wakikamua.

Wanenguaji wa Diamond Musica katika pozi baada ya kushuka jukwaani.

Mnenguaji wa ‘Twanga’ maarufu kwa jina la Sharapova ameingiza tattoo mpya nyuma ya kiuno chake kama anavyoonekana.

Sharapova pichani.



Wanafunzi na walimu wa Shule ya Msingi Kilimani ya Manzese jijini Dar, wakimsikiliza Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya magazeti ya Global Publishers, Richard Manyota (mwenye kizibao) baada ya kutembelea kwenye kampuni hiyo.

0 comments: