MAMA Mzazi wa staa wa maigizo Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila (pichani) amekiri kupata wakati mgumu kumlea mwanaye kiasi cha kukosa usingizi.
Lucresia alisema katika ‘one on one’ na paparazi wetu Jumapili iliyopita kuwa mwanaye anamshinda ujanja, kwani mara nyingi huwa anamwambia anakwenda kwa rafiki zake lakini baadaye inakuja kugundulika kinyume chake.Alisema, magazeti ndiyo humgutusha na kubaini kwamba kumbe mwanaye alimdanganya.
“Anaweza kuniambia anakwenda kwa rafiki yake lakini baadaye nakuja kuona picha gazetini kumbe alikuwa klabu, inanisikitisha hasa kwa sababu nampenda mwanangu,” alisema Lucresia.
Aliendelea kusema kuwa Lulu akiwa nyumbani ni mtoto mzuri, kwahiyo hata habari za kulewa ameziona kwenye gazeti.
Mama huyo aliongeza kuwa havutiwi na skendo za mara kwa mara kuhusu mwanaye, hasa ya ulevi na vitendo vingine vinavyokwenda kinyume na maadili kwenye jamii.Lucresia alisema: “Mara nyingi matukio ya Lulu yanatokea nikiwa safarini, ananipigia simu na kuniambia anakwenda kwa rafiki yake au sehemu yoyote inayokubalika lakini baadaye nasikia tofauti gazetini.
“Ananidanganya, lakini mimi nampenda mwanangu, napenda awe mtu safi kwenye jamii, azidi kufanikiwa kwa kipaji chake, kwahiyo nikiona jambo baya huwa namkanya.”
Aliendelea kusema: “Unadhani kama mtu anakuaga anakwenda kwenye kazi zake za filamu halafu unakuja kuona tofauti utafanya nini? Kwahiyo mimi huwa namkanya ili awe mtoto bora.”Mbali na kauli hiyo, Mama Lulu pia alipiga picha mbalimbali na mwanaye, huku akimkumbatia, hivyo kusherehesha kauli yake kuwa anampenda na ataendelea kumlea katika misingi bora.
Baadhi ya picha hizo, zinaonekana ukurasa wa kwanza wa gazeti hili.
Hata hivyo, kwa upande wa Lulu licha ya kwanba habari nyingi ambazo huandikwa, huambatanishwa na picha halisi za matukio, aliendelea kukanusha kuwa anasingiziwa.
“Unajua mimi ni staa, kwahiyo wakati mwingine nazushiwa ila siyo kweli, habari nyingi siyo za kweli,” alisema Lulu.Gazeti hili, linamtakia Mama Lulu moyo wa subira na ukakamavu ili aweze kumlea mwanaye katika misingi bora, inayompendeza Mungu, mashabiki wa filamu na jamii nzima. MHARIRI.
Wednesday, October 20, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comments:
Pole sana mama Lulu mkabidhi mungu suala hili,mwenyezi mungu ndiye muweza omba/muombee mtoto wako (lulu) kila wakati, kuwa naye karibu, atakuwa mtoto mkweli, mtiifu ataachana na mambo hayo unayoyasikia, huwezi kuamini matokeo yake, bado mtoto japo ana upeo/kipaji mkubwa wa kufanya mambo mazuri ya kijamii katika mambo ya sanaa katika uelimishaji wa jamii. Mama Lulu kuwa karibu na mtoto wako usiwe mkali sana, tumia muda mwingi kuwa naye mueleze hasara zake juu ya hayo matendo mabaya anayoyafanya kama jinsi unavyoyasikia juu yake mara unaporudi kutoka safarini.
Barikiwa!
Nakutakia mafanikio mema usikate tamaa, Usichoke!
Abbie
Post a Comment