Baby Boy katika pozi.
Bwana mdogo anayekuja kasi ndani ya Bongo Flava akitokea ndani ya lebo ya Zizzou Entertaiment, Edson Wilson 'Baby Boy', hatimaye amekutana uso kwa uso na mkali wa miondoko ya Shikide Shikide, Dully Sykes a.k.a Mr Misifa na kufanya singo moja inayokwenda kwa jina la Afternoon. Singo hiyo imefanyika katika Studio za Bongo Records chini ya Prodyuza Paul Matthyasse P.Funk Majani.
Akisema na mateja20 juu ya ujio wa singo hiyo, Baby Boy alisema kwamba kutokana na ladha mpya walizotupia kwenye ngoma hiyo, itabamba si kitoto mara tu itakapoanza kuchezwa kwenye vituo mbalimbali vya Redio na Television na kwamba wimbo huo unachezeka ile mbaya.
Baby Boy aliongeza kwamba nyimbo hiyo mpya itakuwa inakamilisha idadi ya Track tatu tangu aanze game na ndiyo nyimbo pekee inayotambulisha ujio wa albam yake ambayo anategemea itakuwa na jumla ya nyimbo 10 na kuendelea.

0 comments:
Post a Comment