Gea Mbarukh Habib.
Kiti cha Moto ni kiungo muhimu kati ya wasomaji wa Ijumaa Wikienda na mastaa mbalimbali. Kona hii inaweza kumkutanisha staa na ndugu yake waliyepotezana kwa njia rahisi.
Wiki iliyopita kwenye safu hii, tulimuweka Mtangazaji anayesababisha raha kwa msikilizaji ndani ya Redio ya Watu, Clouds FM, Gea Mbarukh Habib. Kama kawa, wasomaji walituma SMS, akapelekewa mwenyewe halafu akajibu moja baada ya nyingine.
Kubwa ni kwamba safu hii imeweza kumkutanisha Gea na Classmate wake. Soma swali na jibu kati ya msomaji na mtangazaji huyo;
Serengeti Boys tena?
Gea upo juu kiutangazaji ila kuna skendo kuwa unapenda Serengeti boys, je ni kweli? Abdi, Dar, 0719463000
GEA ANAJIBU: Mimi nampenda mume wangu mtu mzima.
Changamoto za utangazaji
Gea hongera kwa kuwa mmoja kati ya watangazaji mlio juu kwa sasa, vipi kuna changamoto zozote katika kupata Hekaheka mitaani kwetu? Ongeza bidii, big up. Msomaji, Dar, 0718261447
GEA ANAJIBU: Ugumu upo mwingi sana tu lakini napambana nao.
Ni kweli ana bifu na Dida?
Nakufahamu kama mtangazaji wa Kwa Raha Zetu, vipi bifu lako na Dida linaendelea au mmeamua kuelewana? Nadya Mohamed, 0713736117
GEA ANAJIBU: Sijawahi kuwa na bifu na Dida kwa sababu simjui, namjua kama mtangazaji wa redio nyingine yeyote.
Yeye na Dina ni baabkubwa!
Huwezi kumtaja Gea bila Dina, Leo Tena ni ushahidi tosha lakini nakupongeza unavyosaidia jamii hasa maskini hongera kaza buti. Mud Zangira, Dar, 0754288044
GEA ANAJIBU: Asante.
Huyu anataka kuwa mtangazaji!
Mimi napenda unavyotangaza, mimi napenda kutangaza kama wewe naomba namba yako ya simu. Husna, 0654034560
GEA ANAJIBU: Usijali nitakupigia.
Jamani Gea anajiheshimu
Unajilinda vipi na skendo? Sijawahi kusikia umeandikwa vibaya wala kuvaa nguo za ajabu kama masupastaa wengine inaelekea unajiheshimu sana, Leo Tena ni chachu ya redio zote, wanaiga mfumo wa kipindi chenu hasa Hekaheka kwahiyo nyie mko juu kazi mnaiweza. Msomaji, 0653584034
GEA ANAJIBU: Najiheshimu mimi kama mke wa mtu halafu mama.
Kiti cha Moto chamkutanisha na Classmate wake
Eti wewe Gea ulimaliza Shule ya Msingi Kurasini mwaka 1995,kama kweli tutafutane mimi classmate mwenzako. Martha, 0782254425
GEA ANAJIBU: Kweli, nitakutafuta.
Kwenye tangu mwaka 2001
Hongera kwa kipindi chenu cha Leo Tena, kinatupa raha, je uliolewa mwaka gani na una watoto wangapi? Lono, Dar, 0719143134
GEA ANAJIBU: Niliolewa mwaka 2001, nina watoto wawili.
Msanii apata pakutokea
Napenda sana unavyofunika kwenye kipindi chako ukweli unatisha sana, Gea nina ngoma yangu nikuletee unitwangie? Jailum, Arusha, 0753737270
GEA ANAJIBU: Sawa ilete.
Kumbe Gea wa 1981!
Wewe Gea umezaliwa mwaka gani na umeanza lini kazi ya utangazaji? Mama Elvs, Dar, 0656334307
GEA ANAJIBU: Nimezaliwa mwaka 1981 na kazi nilianza 2004.
Aulizwa haogopi kupigwa?
Swali langu inakuaje kipindi cha Hekaheka huogopi kupigwa?Msomaji, 0715340670
GEA ANAJIBU: Ha ha ha haaa (kicheko), siogopi na kwanini nipigwe?
Vipi mumewe ni babu?
Mbona unapenda kumwita mumeo mzee Habibu au umeolewa na mtu mzima sana? Msomaji, 0752899909.
GEA ANAJIBU: Mume wangu siyo mzee sana wa kawaida tu.
Swali la kifamilia zaidi!
Napenda sana Hekaheka zako, je watoto wako wana umri gani na umeolewa mwaka gani? Mam, Tanga, 0712719978
GEA ANAJIBU: Mtoto wangu wa kwanza ana miaka nane na wa pili miaka miwili.
Gea kiboko ya mashakunaku
Kwa kweli uko juu warekebishe hao washakunaku umewarekebisha sana. Halima Jafari, Dar, 0717309525
GEA ANAJIBU: Asante.
Hata kwa upinde uke wenza hataki
Napenda sana visa vyenu kwenye Leo Tena ila ningependa kujua wewe ni mtoto wa Kiislamu kwanini unakataa unasema hutaki uke wenza wakati dini imeruhusu? Mama Tasha, Dar, 0654817202
GEA ANAJIBU: Kwani ni mambo yote ya dini watu wanafuata mbona Mungu amesema usizini lakini watu wanazini?
Hajui kukasirika jamani!
Gea uko juu, hivi huwa unakasirika? Maana nakupenda naomba unitafute. Mama Doreen, Mwanza, 0767033595
GEA ANAJIBU: Huwa nakasirika kwa sababu mimi ni binadamu, usijali nitakutafuta.
Huyu ishu ya filamu sijui kaambiwa na nani?
Bi Gea Mungu amekujalia umbo na sura nzuri, je umeolewa na una watoto vipi kucheza filamu umeacha?
Faraji Rupia, Tanga,0716454290
GEA ANAJIBU: Sijawahi kucheza filamu.
BIG UP
Nakupa big up sana dada Gea, kifupi napenda unavyotangaza lakini unawezaje kuhimili Hekaheka za mitaani kwa jinsi ulivyo bonge (mnene)? Mwanahamis Sadick, Moro, 0655718882
GEA ANAJIBU: Mimi ni mnene lakini mwepesi ila sijawahi kukimbizwa.
Ugomvi wa mitaani wanahamishia redioni, kweli?
Gea wewe na mtangazaji mwenzako mkigombana na watu mnakuja kujibu kupitia kipindi chenu huoni kwamba mnajishushia hadhi? Mama Habasa, 0786125875.
GEA ANAJIBU: siwezi kubishana na mtu kwenye redio na siyo tu kwenye redio bali hata barabarani siwezi.
Ana ajenda gani na Jahazi?
Kifupi mimi ni shabiki wa Taarab, nilikuwa nataka kufahamu kwanini unapokuwepo kwenye vipindi vya muziki wa taarab unapiga sana nyimbo za Jahazi na za wengine unapiga mara moja moja? Jirekebishe kwani upo juu. Msomaji, 0712140140
GEA ANAJIBU: Wasiwasi wako tu huwa nachanganya zote.
Uhusiano wake na Mishi B vipi?
Gea hivi wewe una undugu na Mishi B? Kwani sauti zenu zinafanana sana. Msomaji, 071293388
GEA ANAJIBU: Sina undugu naye,
Wapi Mamaa Sakina Lihoka?
Nakupa big up kwa kumudu vipindi lakini nahitaji kujua alipo shost wako mwingine ambaye ni Sakina Lihoka. K, Dar, 0712642082
GEA ANAJIBU: Yupo hapa hapa Dar.
Ni Msambaa wa Mazinde!
Ninavyomjua Gea ni Msambaa na kwao ni Mazinde mkoani Tanga na ana watoto wawili. Mary, Dodoma, 0655401360
GEA ANAJIBU: Kweli.
Huyu atakuwa anabahatisha!
Gea amezaliwa Gerezani amekulia Gerezani amesoma Jitegemee lakini mbona siku hizi amekuwa haeleweki? Yakobo, 0757202202
GEA ANAJIBU: Siyo kweli, mimi nimezaliwa Kurasini
PONGEZI
Nakupongeza sana kwenye Leo Tena nakupenda wewe, Dina na Zama napenda wawe kama dada zangu na washauri wangu siyo kwa sababu ya usupastaa hapana naomba unitafute kwa namba yangu. Msomaji, 07558130
GEA ANAJIBU: Sawa.
Hili swali la kikazi zaidi!
Gea napenda sana kipindi cha Leo Tena hivi unavyokwenda kuwahoji watu wanakujua au wanashtukia tu redioni? Rehema Kimambo, Moshi, 0757953584
GEA ANAJIBU: Hapana lazima nimwambie mtu kuwa naongea naye.
Ni mtoto wa marehemu Mbarukhu
Naipenda sauti yako, namjua kama mtoto wa marehemu mzee Mbarukhu wa Mazinde, anao ndugu zake Lushoto Kiwanda cha Chai. Mama Hassan, Dar, 0756233569
GEA ANAJIBU: Kweli.
Adui yake Leo Tena ni nani?
Hivi Gea naomba kuuliza katika kipindi chenu cha Leo Tena kinaonekana kama mnabishana na mtu, je ni nani? Zeana Rummy, Dar, 0715527920
GEA ANAJIBU: Hapana huwa hatubishani na mtu.
Historia yake kwa ufupi
Ningependa kufahamu historia yako kwa ufupi, umezaliwa wapi, elimu yako, umeolewa na una watoto wangapi? Laurian Mboya, Moshi, 0754690657
GEA ANAJIBU: Mimi nimezaliwa Dar es Salaam, elimu yangu ya kawaida tu kidato cha nne, nimeolewa na nina watoto wawili.

0 comments:
Post a Comment