MGOMBEA ubunge wa Bariadi Magharibi kupitia CCM, Andrew Chenge, ameiambia Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kwamba shahidi wa tatu wa upande wa mashitaka ana chuki naye.
“Shahidi huyu alitoa ushahidi dhidi yangu ambao si wa kweli na ni kwa sababu ana ‘bifu’ na mimi,” alisema Chenge akimaanisha kuwa ana chuki naye.
Chenge alitoa kauli hiyo jana mahakamani hapo alipokuwa akijitetea dhidi ya mashitaka yanayomkabili ya kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha vifo vya wanawake wawili katika barabara ya Haile Selassie, Oysterbay, Dar es Salaam.Alidai mbele ya Hakimu Mfawidhi, Kwey Rusema, kuwa ushahidi uliotolewa na shahidi huyo, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Usalama Barabarani wa mkoa wa Kinondoni, Fortunatus Musilim, ni wa uongo.
“Sikuendesha gari kwa uzembe bali dereva wa bajaj ndiye aliyesababisha ajali hiyo, kwa sababu alihama upande wake wa barabara na kuja upande wangu,” alijitetea Chenge.
Upande wa Mashitaka ukiongozwa na Wakili Richard Rweyongeza ulipomwuliza kama anamfahamu Musilim, alikana kumfahamu na kudai kuwa amemwona kwa mara ya kwanza mahakamani hapo akitoa ushahidi ambao aliuita ni vituko.
Katika ushahidi wake, Musilim alidai kuwa eneo ambalo ilitokea ajali hiyo, kulikuwa na kibao cha kudhibiti mwendo kasi, ambapo mshitakiwa huyo alikana kukiona na kudai kuwa ameishi eneo hilo kwa miaka 20 bila kuona kibao hicho.
Aidha, Chenge alikana kugongana uso kwa uso na bajaj hiyo, kama upande wa mashitaka ulivyodai na kuongeza kuwa kama ilikuwa hivyo, basi gari lake lingeumia kwa mbele na dereva wa bajaj asingetoka mzima.
Akielezea tukio hilo, Chenge alidai kuwa ilikuwa ni kati ya saa 8.15 na 8.30 usiku, wakati akirudi nyumbani kutoka mjini na mwendo wa gari lake ulikuwa ni kati ya kilometa 70 na 100 kwa saa, ambapo alikutana na chombo chenye mwanga hafifu kikitokea mbele katika barabara ya Haile Selassie.
Alidai, kuwa alipokaribia aligundua kuwa ni bajaj na magari mengine mawili yaliyompita na ghafla bajaj ilihama na kwenda upande wake na alipojaribu kuikwepa ilishindikana.
“Si kweli kwamba niliendesha gari kwa uzembe na wala sijasababisha vifo vya hao watu, narudia tena bajaj ilikuja upande wangu na nilijaribu kumkwepa, lakini kulikuwa na gari upande wa kulia,” alidai Chenge.
Mbali na hilo, mshitakiwa huyo alikana madai ya upande wa mashitaka, kwamba hakuwa na bima na kuongeza kuwa bima iliyopelekwa mahakamani hapo, ilikuwa na makosa ya uchapaji.
Akisoma vielelezo mahakamani, alidai kuwa hati ya kwanza iliyokuwa imeandikwa namba T 512 AEC si yake na yake ni namba T 512 ACE na ndiyo ambayo alilipia bima.
Hapo awali ilidaiwa kuwa mshitakiwa alikuwa akiendesha gari aina ya Toyota Hilux pick up namba T 512 ACE lililogonga bajaj namba T 736 AXC na kusabisha vifo vya Beatrice Costantino na Vick George.
Musilim ndiye aliyetoa ushahidi kuwa gari la Chenge lilikutwa na mabaki ya ubongo, baada ya kusababisha ajali. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Oktoba 20.

0 comments:
Post a Comment