KITUO cha Televisheni cha Channel Ten na Redio Magic FM vya jijini Dar es salaam vimepata pigo kwa kuondokewa na mmoja wa watangazaji wake mahiri, Abdallah Ramadhani (Pichani) ambaye amefariki dunia katika ajali ya gari Ijumaa wiki hii. Kwa mujibu wa taarifa zinazotolewa na kituo cha Redio cha Magic FM, Abdallah alipata ajali hiyo akiwa njiani mjini Beila, Msumbiji akitoka Afika Kusini kurejea Tanzania Alhamis tarehe 7 mwezi huu. Taarifa zaidi zinasema kuwa marehemu alikuwa kwenye gari aina ya Toyota Prado ambayo ilipasuka tairi la mbele na kupinduka mara kadhaa na hivyo kusababisha kifo chake mara baada ya kufikishwa hospitalini.
Abdallah alikuwa katika mapumziko ambayo aliyatumia kwenda nchini Uingereza kwa siku kadhaa kabla ya kupitia Afrika Kusini ambako alipumzika kwa siku chache na baadae kuamua kurejea nchini kwa njia ya barabara kupitia Msumbiji. Mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo iliyompasua kichwa, familia yake ilifahamishwa ambapo mdogo wake
aitwae Hussein alikwenda kumuangalia hospitali alikolazwa kabla ya kufariki. Abdallah atakumbukwa na watazamaji wa Channel Ten kwa usomaji wake wa taarifa za habari kwa umakini na ufasaha na kwa wasikilizaji wa Magic FM. Uongozi na Wafanyakazi wote wa Global Publishers Ltd unatoa pole kwa wafanyakzi wenzie kwa familia yake kwa msiba huu mzito. SISI TULIMPENDA SANA ABDALLAH, LAKINI MUNGU KAMPENDA ZAIDI YETU NA KAAMUA KUMUITA, AILAZE ROHO YAKE PEPONI - AMEEN!

Enzi za uhai wake.
Hatuko nae tena.
...ndugu na jamaa wa marehemu wakiwa msibani nyumbani kwa marehemu Ilala mtaa wa Kilosa jirani na Makao Makuu ya NCCR Magaeuzi kama walivyokutwa na mtandao huu mapema leo.
..msanii wa filamu 'Baba hajji' (kushoto) akiongea na baadhi ya wafiwa msibani leo.
0 comments:
Post a Comment