Baadhi ya vyombo vilivyotolewa nje na mabaunsa.
WAPANGAJI wa nyumba iliyopo kwenye kiwanja namba 499, Mtaa wa Tosamaganga, Masaki, jijini Dar es Salaam mkabala na kituo Tanesco, jana walipatwa na wakati mgumu baada ya kutupiwa vyombo vyao nje kufuatia aliyekuwa mwenye nyumba wao, Mohamed Hussein, kushindwa kesi katika Mahakama ya Nyumba iliyokuwa ikishughulikia mgogoro wa nyumba hiyo dhidi ya Bains Singh.
Wakazi wa nyumba hiyo wakiwa hawana pa kwenda.
Watoto wakiwa hawajui la kufanya.
Mkazi wa nyumba hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Richard Kyaraa akielezea kilio chake kufuatia kuhamishwa bila notisi ambapo alidai katika uhamishwaji huo ameibiwa shilingi milioni tano na waliohusika kutoa vyombo vyake nje.
Kyalaa akiangalia baadhi ya vitu vyake.
Mashuhuda nao walikuwepo.
0 comments:
Post a Comment