Social Icons

Friday, September 24, 2010

BLACK SUNDAY YAZINDULIWA!!!

MKURUGENZI wa kampuni ya Pili Pili Entertainment (katikati) Sameer Srivastava akimpongeza nyota mmojawapo wa filamu mpya iliozinduliwa usiku wa leo iitwayo Black Sunday,ndani ukumbi wa cinema wa Mlimani City,Steven Kanumba kwa kuonyesha umahiri wake mkubwa wa kuigiza ndani ya filamu hiyo iliokuwa na msisimko mkubwa kwa watazamaji. Mbali ya Kanumba pia kulikuwepo na nyota wengine walioinogesha filamu hiyo vyema kama vile Aunt Ezekiel,Monalisa,Yusuph Mlela na wengineo.Uzinduzi wa filamu hiyo uliandaliwa na kampuni ya Pili Pili Entertainment na kuhudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali.
Nyota wa filamu ya Black Sunday iliozinduliwa usiku wa leo,Steven Kanumba akibadilishana mawazo na baadhi ya wageni waalikwa waliofika kwenye uzinduzi wa filamu hiyo iliokuwa na waigizaji wenye vipaji kibao, mara baada ya kutoka kuitazama.
Wageni waalikwa wakiingia kwenye ukumbi kuishuhudia filamu hiyo usiku huu.
Wadau mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuingia ndani ya ukumbi husika kuishuhudia filamu hiyo ya Black sunday,ambayo kiukweli imejawa na matukio ya kusisimua.
Pichani kushoto ni mdau Hala hala akiwa amepozi na Mkurungenzi wa kampuni ya Pili Pili Entertainment (katikati) Sameer Srivastava pamoja na Mdau mwingine wa mambo ya filamu.
Slyvia na rafiki yake wakiwa wamepozi mbele ya kamera ya Jiachie usikuu
Wadau wakitoa mawazo yao mbalimbali kabla ya kwenda kuitazama filamu yenyewe.
Mtangazaji wa Clouds Tv kupitia kipindi chake cha Take One,Zamaradi Mkeketema akifanya mahojiano mafupi na Rais wa shirikisho la wasanii wa Filamu Tanzania,Bw.Simon Mwakifwamba.
Shoto ni Muigizaji mkongwe wa filamu hapa nchini,Mzee Chilo,Yusuph Mlela pamoja na mmoja wa wageni waalikwa wakijadiliana jambo kwa umakini usiku huu kabla ya uzinduzi wa filamu ya Black Sunday uliondaliwa na kampuni ya Pili pili Entertainment.
Wasanii mahiri wa filamu wakifafanua jambo mbele ya TBC1 kuhusiana na uzinduzi wa filamu hiyo mpya.
Dr Cheni ambaye pia ni muigizaji mahiri katika filamu haoa nchini akifanyiwa mahojiano mafupi na mtangazaji wa Star TV Sauda Mwilima kuhusiana na uzinduzi wa filamu hiyo mpya ambayo imerekodiwa kwa umahiri mkubwa na yenye matukio ya kusisimua.
Kanumba na mdau mgeni mwalikwa wakibadilisha mawazo.
Wadau mbalimbali waliofika kwenye uzinduzi wa filamu hiyo mpya ya Black Sunday,wakibadilisha mawazo kabla ya kwenda kuitazama.
Vincent Kigosi.a.k.a Ray akifafanua jambo kwa umakini kabisa.
Wageni waalikwa mbalimbali walichangia mawazo yao kuhusiana na tasnia nzima ya filamu hapa nchini.,Mzee Chilo,Slyvia pamoja na Zamaradi Mketema katika pozi la picha
Slyvia akiwa amepozi na mgeni mwalikwa usiku wa leo
Mbunifu mahiri wa mavazi hapa Bongo,Ally Rhemtullah nae akizungumza machache kuhusiana uzinduzi huo ulionekana kufana sana usiku wa leo.
Wadau mbalimbali wa filamu wakiwa wamepozi kwa pamoja mbele ya kamera jiachie usiku huu.
Wadau mbalimbali wakiendelea kuwasili kwenye uzinduzi wa filamu mpya ya Black Sunday uliondaliwa na kampuni ya Pili Pili Entertaiment na kuhudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali.
Mkurungenzi wa kampuni ya Pili Pili Entertainment (katikati) Sameer Srivastava akifanyiwa mahojiano mafupi kuhusina na maandalizi ya uzinduzi wa filamu mpya ya Black Sunday usiku huu ndani ya Mlima City.

PICHA:MICHUZIJR BLOG

0 comments: