Social Icons

Wednesday, September 22, 2010

TIGO YAZINDUA TAWI JIPYA TEMEKE

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Chiku Gallawa akikata utepe kuzindua rasmi kituo cha huduma kwa wateja cha Tigo, Temeke eneo la Mtoni kwa Aziz Ali jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Ofisa Uhusiano wa Tigo,Jackson Mmbando na wanne kushoto ni Meneja Matawi ya Tigo, Innocent Mayawa.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Chiku Gallawa (kushoto) akijisajili na huduma ya Tigo Pesa muda mfupi baada ya kuzindua Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Tigo, Temeke, Dar es Salaam jana. Kulia ni Ofisa Huduma kwa Wateja wa kituo hicho, Josephine Reuben wa pili kushoto ni Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Jackson Mmbando na katikati ni Meneja Matawi wa Tigo, Innocent Mayawa.

fisa Huduma kwa Wateja wa Tigo, David Kagusa (kulia) akikabidhi zawadi kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Chiku Gallawa mara baada ya mkuu huyo kuzindua kituo cha Huduma kwa Wateja cha Tigo, Temeke, Dar es Salaam.


0 comments: