Social Icons

Friday, September 17, 2010

MASHINDANO YA POOL YA SHIKA KASI ARUSHA

Baadhi ya washiriki kutoka mikoa mbalimbali wakiwasili ndani ya ukumbi wa Matongee, Jijini Arusha tayari kwa michuano hiyo ya Pool.
Mashindano ya taifa ya mchezo wa pool yamefunguliwa rasmi mkoani Arusha na timu kumi na nne kutoka mikoa tofauti ya Tanzania Bara inashiriki fainali hizo.
Fainali hizo zimedhaminiwa na bia ya safari lager ikiwa ni ishara ya kuendeleza mchezo wa pool ambapo mkoani Arusha yanafanyika katika ukumbi wa Matongee.
Mashindano hayo yanashirikisha wachezaji wanawake na wanaume ambapo mchezaji wa kike atakayetwaa ubingwa wa mashindano hayo atashiriki katika mashindano ya dunia yanayotarajia kufanyika nchini UFARANSA mwaka huu.
Na Jane John Blog.

0 comments: