Hakika kifo hakina huruma wala saa hata notisi.Kilichomtokea mzee huyu leo asubuhi pale pande za Ubungo Bus Terminal kinasikitisha sana. Mzee wa watu, ametoka nyumbani kwake asubuhi na mapema kuelekea kwenye kituo cha mabasi kwenda huko alikokuwa amepanga kuwa mgeni au kureja nyumnani kwake siku ya leo, bila kujua kuwa Mungu amempangia kifo chake leo kabla ya jua kuchomoza. Mzee, huyu ambaye hakutambulika mara moja, amegongwa na basi la abiria liendalo mikoani wakati likitoka lango kuu kwenda na safari zake, tairi lilipanda mwilini mwa mzee huyu na kumuua hapohapo akiwa ameshika mkoba wake wa safari mkononi. Hivi sasa tunavyosoma habari hii ya kusikitisha mwili wake uko mochwari katika hospitali ya Mwananyamala na kwa yeyote anayemfahamu ajitokeze, nahisi familia yake haina taarifa. Mungu alitoa na YEYE ametwaa mja wake, YEYE ndiye Mfalme wa Mbingu na Ardhi na KWAKE sote tutarejea!! Ailaze roho ya Marehemu Peponi - ameen!
umati wa wasafiri na wapita njia wakishuhudia mzee wa watu akiwa hana kauli tena
...basi la kushoto (ambalo halikuweza kujulikana mara moja) ndilo lililohusika na ajali hiyo. Dereva wake alijisalimisha mikononi mwa polisi, ingawa basi liliruhusiwa kuendelea na safari zake.
..askari polisi wakisaidiana na raia kumpakia marehemu garini
...maiti ikipelekwa kuhifadhiwa Mwananyamala hospitali.
0 comments:
Post a Comment