Baadhi ya viongozi wa mashirikisho ya wasanii nchini wakifuatilia mada
kuhusu namna ya kuandaa Mpango Mkakati iliyokuwa ikiwasilishwa na Mwalimu
Rashid Masimbi (Hayupo pichani) wa Kituo cha Sanaa za Maonyesho Tanzania.
Mzee Nkwama Bhalanga ambaye ni Mjumbe Kwenye Shirikisho la Sanaa za
Ufundi akichangia moja ya mada zilizowasilishwa kwenye semina hiyo.
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania,Che Mundugwao
alisisitiza kwamba, ni muda wa wasanii kutetea haki zao kupitia
mashirikisho waliyounda.Alihimiza wasanii kuunda umoja wao.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria semina hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka viongozi wa mashirikisho ya
wasanii kuhakikisha wanakuwa imara na thabiti ili kuleta ufanisi kwenye
mashirikisho ya wasanii nchini yaliyoundwa na kupata viongozi wake hivi
karibuni.
Hayo yamesisitizwa na Wakufunzi kutoka BASATA wakati wakitoa semina kwa
viongozi wa mashirikisho ya wasanii nchini iliyofanyika wiki hii kwenye
ukumbi wa Baraza hilo na kuhudhuriwa na viongozi wote wa mashirikisho ya
wasanii na wajumbe wao.
Mashirikisho yaliyohusika kwenye semina hiyo ni pamoja na lile la Sanaa ya
Muziki,Maonyesho,Ufundi na Filamu ambapo mada mbili zilizotolewa kwa
viongozi hao ambazo ni Wajibu na Maadili ya Uongozi wa Mashirikisho ya
Sanaa iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Mfuko na Uwezeshaji wa
BASATA,Bw.Ruyembe Mulimba na na ile ya Mchakato wa Kuandaa Mpango Mkakati
wa Shirikisho iliyowasilishwa na Mwalimu Rashid Masimbi kutoka Kituo cha
Sanaa za Maonyesho Tanzania.
Akizungumza kwenye semina hiyo,Ruyembe alisema kwamba, viongozi wa
mashirikisho ya wasanii hawana budi kuwa mstari wa mbele katika kutetea
maslahi ya wasanii,kuwa na mwenendo mwema, kuzingatia maadili ya uongozi,
kuzingatia dhana ya kutangulia na kuelekeza huku mtangulizi akiwa
anafahamu anakowapeleka watu anaowaongoza.
“Kiongozi mzuri lazima aelewe majukumu na mwenendo mwema katika kazi ya
kusimamia watu ambao wanahusika na utendaji wa shughuli husika kwa
ushirikiano na kwa pamoja kulingana na Katiba iliyopo” alisisitiza
Ruyembe.
Aliongeza kwamba, historia inaonesha vyama vingi na shirika za wasanii
zimekuwa kwenye migogoro isiyoisha kutokana na viongozi kutokuwa na utashi
wa kuongoza., kutanguliza maslahi binafsi na kushindwa kabisa kuwa na
maono ya kutekeleza mikakati inayokuwa imewekwa.
Alizidi kufafanua kwamba, wasanii wanakumbwa na changamoto nyingi sana
zikiwemo za wao kuibiwa kazi zao, kunyonywa kupitia mikataba, kulipwa
malipo kidogo na ukosefu wa masoko hivyo viongozi wa mashirikisho hawana
budi kuwa mstari wa mbele kuhakikisha changamoto hizo zinawekewa mikakati
ya kupunguzwa kama si kumalizwa kabisa.
Naye Mwalimu Rashid Masimbi alisema kwamba, moja ya kazi ya viongozi hao
wa mashirikisho ya wasanii ni kuhakikisha wanakuja na Mpango Mkakati wa
muda mfupi na mrefu ambao utalenga kujenga dira ya utendaji na mafanikio
ya mashirikisho.
Aliongeza kwamba, viongozi hawana budi kuwa na mpango mkakati ambao
utaeleza nini kitafanyika,nani atakifanya, kwa namna gani na kwa muda
gani.
“Mpango Mkakati ndiyo dira, dhamira, malengo, shughuli na matokeo ya
utendaji wa shirikisho lolote hivyo lazima nyinyi viongozi mtuoneshe ni
kwa jinsi gani tutayafikia haya” alisisitiza.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria semina hiyo waliishukuru BASATA kwa
mpango huo na kusisitiza kwamba, semina kama hizo ziandaliwe mara kwa mara
ili kujenga ufanisi wa mashirikisho ya wasanii na sekta ya sanaa kwa
ujumla.

0 comments:
Post a Comment