Social Icons

Friday, August 13, 2010

SHAMSA FORD: NAPENDA RANGI YA ZAMBARAU, HATA ‘KUFULI’ LANGU NI RANGI HIYO!

Kutoka pande hizi za Ten Question wiki hii tunamleta kwenu sistaduu anayekuja juu kwa kasi ndani ya Kiwanda cha filamu Bongo, Shamsa Ford ambaye alizaliwa miaka 23 iliyopita, mwenye asili ya kabila la Kihehe aliyekulia jijini Dar maeneo ya Sinza Afrikasana yalipo makazi ya wazazi wake. Kielimu Shamsa aligonga Shule ya Msingi Mapambano iliyopo Sinza na baadaye alijiunga na Shule ya Sekondari ya Kunduchi Beach kabla ya kwenda kidato cha Tano na Sita huko kwa Rais Museven Uganda katika Shule ya Budo. Staa huyu anasema kati ya vitu alivyokuwa akivihofia alipokuwa skuli ni tishio la majini ambalo lilipewa kipaumbele na kusababisha wanafunzi wengi kukosa masomo katika shule alizosoma. Ili kujua ‘deteili’ zake kiundani, tambaa na Ten Questions zilizomtoa jasho.

TQ: Unaweza kukumbuka ni lini na ilikuwaje ukajiunga na fani ya filamu?

Shamsa: Fani ya uigizaji ilitokana na kujiamini kwangu na asikwambie mtu nilikuwa natamani sana kupata nafasi kwani nilijua nina kipaji cha uhakika. Nakumbuka presenta Zamaradi Mketema wa Clouds FM ndiye aliyeniunganisha na jamaa fulani ambapo nilifanya filamu ya Endless Love ambayo bado haijaingia kitaani ‘but’ huko ndiko nilikopata ‘chansi’ ya kukutana na waigizaji wakubwa kama Ray na Kanumba ambapo nilifanya nao kazi na namshukuru Mungu walinikubali. Nikiwa na Ray nilifanikiwa kugonga filamu ya Saturday Morning na baadaye niliingia kwa Kanumba ambaye naye hakunibania hivyo nimeshafanya nao filamu kibao, zingine ziko sokoni na mzigo mwingine mkubwa unakuja.

TQ: (swali la Kikorombwezo) Umeolewa?
SHAMSA: Sijaolewa ‘but’ nina mchumba ambaye tulikutana tangu nikiwa kidato cha tano na ndiye mtu wangu wa kwanza na wa mwisho. Tayari amenivisha ‘engagement’ na mipango kabambe ya kufunga ndoa ya kihistoria inaendelea. Ni mapema sana kuwatajia mwenye mali ‘coz’ nataka iwe ‘sapraizi’, lakini nitawaalika. Mjue tu anaanza na herufi D, ni mtu na biashara zake. Jamaa hana ujanja kwangu, kafa kaoza.

TQ: Mchumba wako anapenda kazi unayofanya ya uigizaji?

SHAMSA: Anaipenda kwani hajawahi kuniambia kama haipendi, ni mtu muwazi ‘so’ kama angekuwa hapendi angenieleza.

TQ: Katika uigizaji wanaume wengi wanakuona na wangetamani ‘kutoka’ na wewe. Je, unapata usumbufu wowote kutoka kwa wanaume wa aina hiyo?
SHAMSA: Usumbufu upo sana lakini nina wangu ambaye kamwe siwezi kuingia mkenge.

TQ: Skendo yako ya kwanza ni kutwangana na mwigizaji mwenzako aitwaye Maya, ambapo baadaye ilibainika kuwa mlikuwa mnamgomea staa mkubwa, mwanaume wa filamu hapa nchini. Je, hili likoje?
SHAMSA: Ugomvi wangu na Maya hakumhusisha mwanaume ila tulitofautiana katika mambo binafsi ambayo siwezi kuyasema hapa.

TQ: Kuna kasumba kuwa wacheza filamu wanatumia bangi, sigara na madawa ya kulevya ili kuvuta ‘stimu’ za kuigigiza. Je, kwa upande wako hali ikoje?


SHAMSA: Situmii vitu hivyo kabisa na huwezi amini hata pombe sinywi. Kama sehemu ninayotakiwa kuigiza inayohitaji ‘mudi’ fulani, huwa namwomba ‘direkta’ ananipa muda wa robo saa ‘then’ nakuwa katika hiyo hali inayotakiwa.

TQ: (swali la kifuta jasho) Unapenda rangi gani?
SHAMSA: Rangi yangu ni zambarau kuanzia nje mpaka ndani, namaanisha kuanzia gari, nyumba na nguo. Hata ‘kufuli’ ni rangi hiyo hiyo.

TQ: Mafanikio vipi?
SHAMSA: Mbali na vitu vinavyoonekana, lakini nimejuana na watu wengi hasa wale wenye majina makubwa ambao hata nikikaa nao, napata mambo ya kunijenga kimaisha. Siku moja nilipigiwa simu na rafiki yangu baada ya kuniona kwenye filamu ya Saturday Morning, nilipofika nyumbani kwao, mama yake alifurahi sana na akaniambia yeye anaishi Marekani lakini huwa hakosi filamu za Kanumba hivyo alinipongeza na wakati wa kuondoka alinipa zawadi kibao na fungu la ‘mapene’ ambalo hadi siamini ‘coz’ lilikuwa kubwa.

TQ: Ni vikwazo gani unavyokumbana navyo katika kazi yako ya uigizaji?

SHAMSA: Vikwazo ni vingi ‘but’ bidii na kujituma katika kazi ndiyo kila kitu.

TQ: Nini matarajio yako ya baadaye?
SHAMSA: Tayari mipango ya kwenda kusoma nchini Uganda katika Chuo cha Makerere imekamilika, nakwenda kusoma Mawasiliano ya Umma ‘Mass Communication’ ili kunipa nafasi zaidi ya kujipambanua katika sanaa kisomi zaidi.






0 comments: