Akiongea na mwandishi wa mtandao huu, Mkurugenzi wa mashindano hayo, Rita Paulsen, alisema kwamba usaili huo ulianza na washiriki 600 tangu Agosti 10 mwaka katika fukwe hizo. Kufikia leo wana idadi ya washiriki 1,200 na baadhi yao wameshaanza kuchujwa tayari kwa kutafutwa washindi ishirini watakaoingia hatua ya kwanza, kabla ya kuchujwa tena mwishoni mwa wiki hii ambapo watapatikana 10 au 18 watakaoingia kambini tayari kwa kuchuana na waliopatikana mikoani.
Kushoto ni mmoja wa washiriki wa kinyang’anyiro hicho mwenye namba BSS 1046 akiandikisha jina lake tayari kwa usaili, na kulia ni mratibu wa mchakato huo akiandika jina la mshiriki huyo.
Baadhi ya washiriki wakiwa wamepozi tayari kwa kusubiria zoezi
Washiriki wa zoezi
Mshiriki namba 1042 “akichana mistari” ndani ya chumba cha usaili.
Baby Jacob mwenye namba 1043 akionyesha mbwemwe zake kwa majaji.
Jopo la majaji likiongozwa na Rita (katikati) na kushoto kwake ni Master J na mwisho kushoto ni mmoja wa majaji hao.
0 comments:
Post a Comment