Social Icons

Monday, August 23, 2010

AFRICAN UNIT OF TALENT YAZINDULIWA

KUNDI jipya la sanaa za maigizo nchini, African Unit of Talent, limezinduliwa usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya kisasa ya The Atriums iliyopo Sinza Afrika Sana jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi wa shughuli hiyo alikuwa mkuu wa shule ya Dar City College, Idrisa Mziray.
Akiongea katika uzinduzi huo mkurugenzi mlezi wa kikundi hicho Roger Moshi alisema kwamba ameamua kuzindua kundi hilo ili liwe rasmi kwa wadau wake.
Aidha aliongeza kwamba kutokana na uwepo wa kundi hilo itakuwa ni njia mojawapo ya kuinua vipaji vya wasanii wachanga na njia moja wapo ya kuwapatia ajira.

Baadhi ya wanakikundi wakifuatilia kwa makini zoezi zima la uzinduzi huo.

Mshereheshaji wa shughuli hiyo akipiga mnada moja ya mikoba iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili ya hafla hiyo.

Mmoja wa wana kikundi akisoma risala.
Mziray (aliyesimama katikati) akizungumza machache katika uzinduzi huo. Kushoto kwake ni Nasreen Komba na kulia kwake ni Mkurugenzi Mlezi wa kundi hilo, Roger Moshi na Ofisa wa Dar City College, Chomoka Seif.
Wanakikundi wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Mkurugenzi wa African Unit of Talent Roger Moshi (kulia)akiwa kwenye picha ya pamoja na Wabura mmoja wa wasanii wa kundi hilo.
Baadhi ya wasanii wa kundi hilo wakiwa kwenye picha ya pamoja muda mfupi baada ya uzinduzi huo.Wasanii hao wakijaribu kuigiza moja ya mchezo waliyokwisha kuuandaa.

0 comments: